Baadhi ya viongozi kutoka katika halmashauri za mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha mipango mikakati cha halmashauri. |
Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha zimehamasishwa
kutenga maeneo maalumu kwaajili ya ujenzi wa viwanda kama maelekezo ya serikali
ya awamu ya tano yanavyoelekeza.
Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
alipokuwa akizungumza na viongozi wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha kwa
lengo lakuweka mikakati yakiuntendaji hasa kwa mwaka wa fedha unaokuja
2017/2018.
“Nazitaka halmashauri zote zieleze hapa namna
zilivyojipanga kwa mwaka wa fedha ujao katika kutekeleza adhima ya serikali ya
viwanda,bainisheni maeneo mliyotenga na muelezee hali ya miundo mbinu ya msingi
ilivyo,lina ukubwa gani,lina hati au halina hati na niaina gani ya kiwanda
mmependekeza.”
Aidha amewata watumishi wote wa serikali kubadilika kwa
kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake kila mtu afanye kazi kwa bidii hasa
kwakutekeza malengo ya serikali.
Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambae atakwamisha
malengo ya serikali hivyo hatua zakitumishi zitatumika kwa mtumishi huyo ili
kukuza ufanisi sehemu za kazi.
Gambo anaendesha kikao cha siku 3 kwa kupitia mipango
mbalimbali yakila halmashauri nakushauri nini kifanyike kwa mwaka wa fedha
ujao.