RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Showing posts with label Elimu. Show all posts
Showing posts with label Elimu. Show all posts

Wednesday, November 14, 2018

KILA HALMASHAURI ITENGE SHILINGI 1000 KWA KILA MTOTO WA CHINI YA MIAKA 5

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameziagiza halmashauri zote za mkoa huu kutenga kiasi cha shilingi 1000 kwa kila mtoto katika halmashauri kutoka katika mapato ya ndani ilikusaidia katika mfuko wa Lishe wa halmashauri.

Yamesemwa hayo na katibu tawala wa Mkoa Richard Kwitega kwa niaba ya mkuu wa mkoa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya namna ya upangaji wa bajeti ya lishe katika mkakati wa lishe Kitaifa, amesema hali ya udumavu katika mkoa si nzuri sana upo kwa asilimia 36.

Amesema wahanga wakubwa ni watoto na wanawake ambapo watoto wengi wanaudumavu wa akili na mwili na wanawake wajawazito hujifungua watoto njiti au hupoteza maisha kabisa.

Hali za watoto kwa mkoa wa Arusha  kwa mwaka 2015/2016 watoto  wenye uzito mdogo kwa urefu ni  asilimia 6.5 na wenye uzito mdogo kwa umri ni asilimia 20.1 na watoto 57 kati ya 100 wana upungufu wa damu.
Amesema hali hii pia kwa akinamama wajawazito sio nzuri kwani wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 17, 14 kati ya 100 wana upungufu wa damu kwa takwimu za mwaka 2015/2016.

Akisisitiza zaida mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amesema ifike wakati sasa elimu itolewe kwa kina juu ya ulaji mzuri wa vyakula mbadala vitakavyo ongeza virutubisho mbalimbali katika mwili badala ya kutumia madawa kwa wingi.

Amesema vyakula kama mbogamboga, matunda na vyakula vya nafaka vinavyoongeza madini, vitamin na virutubisho vingine mbalimbali yanayoitajika mwilini.

Pia, mpango mkakati wa lishe unaitaji bajeti ambayo utasimamia utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa, amesema mafunzo hayo waliyopatiwa yatawasaidia kuwa na uwelewa mpana wa namna ya kusimamia shughuli nzima za lishe katika wilaya zao kwa ufasa.

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kutengeneza bajeti za lishe katika mkoa wa Arusha  yaliyosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yalifanyika kwa kuhusisha wilaya mbili ya Jiji la Arusha na Arusha Vijiji na kuendelea katika wilaya nyingine za Meru, Longido,Monduli,Karatu na Ngorongoro.


Wednesday, October 10, 2018

TAIFA LISILO NA UTAMADUNI NI TAIFA LILILOKUFA

Katibu mkuu wa wizara ya habari,Utamaduni,sanaa na michezo, Suzan Mlawi amesema,Taifa lisilo na utamaduni ni taifa linalokufa na kutoa kizazi kisichoweza kuenzi na kuthamini mila na desturi zao.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua tamasha la Urithi wa Utamaduni katika mkoa wa Arusha lililoanza Octoba 8, 2018 hadi Octoba 13 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

“Nimefarijika kuona tamasha hili litakuwa linafanyika kila mwaka, kwani litatoa nafasi kubwa sana kwa watanzania kujifunza tamaduni mbalimbali na pia litaenzi mila na desturi zetu kwa kiasi kikubwa”,alisema.

Amesema kupitia tamasha hili anategemea kuona ukuaji wa uchumi kwani bidhaa nyingi za asili zitapata masoko,kufufua mila na desturi zilizokufa kwa vijana wa sasa.
 Mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi  Pro.Audax Mabula, amesema tamasha hili lilizinduliwa mnamo Septemba 15,2018 na makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu Hasan mjini Dodoma na kuendelea  Zanzibar, Dar es Salaam na sasa lipo mkoani Arusha.

Amesema lengo kubwa la tamasha hili ni kuenzi mila na malikale za Kitanzania kwani ni kwa mda mrefu sasa  utamaduni wa watalii ndio umekuwa ukipewa kipaombele zaidi kuliko huu utalii wa utamaduni.

Kupitia tamasha hili la urithi wa utamaduni itasaidia kuutambulisha zaidi urithi wa utamaduni katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

 Nae katibu tawala wa mkoa wa Richard Kwitega amesema tamasha hili kwa mkoa wa Arusha litasaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mila na desturi za makabila ya mkoa huu na pia kuwakutanisha makabila mbalimbali na kuweza kujifunza tamaduni zetu.

Tamasha hili la urithi wa utamaduni lilizinduliwa kwa mala ya kwanza nchini jijini Dodoma na litakuwa likifanyika kila mwaka kwa mwezi mzima wa Septemba katika mikoa mbalimbali na kwa Mkoa wa Arusha linafanyika pia katika wilaya ya Karatu.






Monday, August 13, 2018

VIJANA SHIRIKINI KATIKA KUJENGA UCHUMI WA VIWANJA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Antony Mavunde akiteta jambo na mwakilishi Mkazi kutoka UNFPA  Bi.Jaqueline Mahon,katika kilele cha siku ya vijana,Meru Arusha.

Bilioni 15 zitatumika  kukuza ujuzi kwa vijana zaidi ya milioni 4.4 nchini, ili kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za uchumi wa viwanda.
Yamesemwa hayo na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, sera,bunge,ajira,vijana na wenye ulemavu Mheshimiwa Antony Mavunde,alipokuwa akihutubia vijana katika kilele cha ziku ya vijana kimataifa Mkoani Arusha.
“Vijana mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za ukuzaji wa uchumi wa viwanda“.
Serikali imeshaweka kipaombele katika kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwapa uwezo wakushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kuwasaidia kukuza uchumi wao.

 Amesema ukosekanaji wa ujuzi ndio changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi kwa sasa, kwani tafiti za  mwaka 2014 zinaonesha kuwa 3.5% ya watu wana ujuzi wa juu, 16.6% wana ujuzi wa kati na 76.9 wana ujuzi wa chini kabisa.

Amesema viwango vya kimataifa vinatambua ujuzi katika 12% uwe wa juu,34% wa kati na 54% niwa chini, hivyo nchini yetu bado inakazi kubwa sana katika kuhakikisha tunafikia kiwango hicho cha kimataifa.

Amewasisitizia vijana wote nchini kuakikisha wanatunza afya zao kwani bado kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kipo kwa vijana.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewataka vijana wasikubali kutumika na watu kwa mambo mbalimbali kama yakisiasa, amesema vijana wanatakiwa kuwa makini katika maamuzi wanayoyataka kuyafanya ili waweze kuamua vitu vyenye tija.

Vijana wakiingia katika viwanja vya chuo cha Patandi kwa Maandamano katika kilele cha siku ya vijana duniani,Arusha.

 Gambo amesema mkoa unaendelea kusimamia shughuli na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na serikali ya awamu hii ya tano.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambae ndie alikuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ya kilele cha siku ya vijana, amesema wilaya yake imeshatenga ekari 3000 kwenye eneo la Malula kwa ajili ya uwekezaji na vijana ndio watapewa kipaombele cha kupewa maeneo hayo.

Ameishukuru serikali ya Mkoa kwa kuleta maonesha hayo katika wilaya yake na amesema wananchi wa Arumeru wamefurai na wamepata elimu ya kutosha.

Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa yalianzishwa rasmi na umoja wa mataifa kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana kujadili maswala mbalimbali yanayowahusu na kuyatafutia majibu na huanzimishwa kila mwaka Agosti 12 ambapo mwaka huu 2018 yameadhimishwa Mkoani Arusha.

Mheshimiwa Antony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya DSW bwana Peter Owaga katika kilele cha siku ya vijana,Arusha.


Friday, July 20, 2018

SHULE ZILIZOIBUKA KIDEDEA MATOKEO KIDATO CHA SITA


Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mkoani Arusha  imefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita  kwa kushika nafasi ya  pili kitaifa kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo, huku shule ya Sekondari Kibaha ikishika nafasi ya kwanza na shule ya Sekondari Kemebos ikishika nafasi ya tatu,hii ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani Taifa.
Aidha matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri ni mwendelezo wa historia ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa ,ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza,mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa kwa watahiniwa wake 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili.
Nuru ya shule hii ya Sekondari Kisimiri yazidi kuangaza kwenye Mkoa wa Arusha wenye shule 17 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na Binafsi 14.Shule zenye watahiniwa chini ya 30 kwa mkoa wa Arusha zipo 13 ikiwa shule 1 tuni ya serikali na 12 ni binafsi.
Ufahuru huu umepelekea Mkoa wa Arusha kupata shule nyingi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita,mbali na Kisimiri shule nyingine 10 zilizofanya vizuri  zenye watahiniwa zaidi ya 30 ni;Iluboru,Embarway,Mlangarini,Gawako,Loliondo,Engutoto,Irikisongo,Maji ya chai,Nainokanoka.Shule iliyofanya vizuri yenye watahiniwa chini ya 30 ni Mwandet.
Hata hivyo baadhi ya  shule katika Mkoa wa Arusha zinatakiwa kuongeza juhudi katika kuinua kiwango cha ufauru nazo ni; shule ya sekondari Florian na Makiba.


Friday, July 13, 2018

MIMBA MASHULENI ZAKITHIRI

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo (wa katikati) akiwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Bwana Gift Kyando wakimsikiliza mwalimu  Mary Marimo akifafanua namna wanavyowafundisha watoto alama za barabarani katika halmashauri ya Monduli.



Viongozi wa Kata wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha watakiwa kutafuta suluhu ya tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Akitoa maagizo hayo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo katika kuhadhimisha siku ya kilele cha wiki ya elimu Mkoani Arusha.

Amesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya elimu Mkoani Arusha ni mimba kwa wanafunzi hasa wa Sekondari,ambapo kwa mwaka 2017 wanafunzi 237 waligundulika kuwa na ujauzito ikiwa wanafunzi 50 ni wa shule za Msingi na 187 ni wa Sekondari.

Aidha,kuanzia Januari hadi Aprili 2018 jumla ya wanafunzi 97 waligundulika kuwa na ujauzito ambapo wanafunzi 17 niwa shule za Msingi na 80 wa Sekondari.

“Bado tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni changamoto kubwa hasa wa sekondari,wazazi bado mna jukumu kubwa hasa la kuhakikisha mnasimamia maadili ya watoto wenu na pia kuchangia fedha za chakula mashuleni ilikupunguza vishawishi kwa wanafunzi hawa”.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akiwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu  Gift Kyando na Katibu Tawala wilaya ya Karatu Abas Kayanda wakipata maelekezo ya elimu vitendo kutoka kwa mwanafunzi Omary Ally wa shule ya Mwalimu Anna iliyopo wilayani Monduli .



Katibu Tawala msaidizi upande wa elimu bwana Gift Kyando,amesema changamoto nyingine iliyopo katika sekta ya elimu Mkoani Arusha ni baadhi ya watoto kutojua kusoma,kuhesabu na kuandika (KKK), kwa sababu watoto hao hawapatiwi elimu ya awali kwanza kabla ya kujiunga na elimu ya msingi.

Amesema mbali na changamoto hizo,elimu bure kwa Mkoa wa Arusha imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya uwandikishaji wa watoto darasa la kwanza.

Akisisitiza zaidi anasema mradi wa mpango wa kusaidia kusoma,kuandika na kuhesabu (LANES) umeweza kusaidia sekta ya elimu kwa kiasi kikubwa kwani mradi umeweza kuongeza Vitabu,Vifaa vya kufundishia na Vyombo vya usafiri,ambapo kila halmashauri itapatiwa kopyuta 3 za kusaidia utunzaji wa taarifa mbalimbali za wanafunzi.

Mkuu waWilaya ya Karatu Theresia Mahongo akimkabidhi mkuu wa shule ya Bwawani mwl. Revocatus Mmary Kopyuta zilitolewa kutoka kwenye mradi wa LENSI.

Juhudi kubwa inaitajika katika kutoa kipaombele kwa watoto wenye ulemavu, kwani Mkoa unajumla ya watoto wenye ulemavu 614 ambao wanaitaji kuwa na madarasa maalumu lakini pia bado kuna baadhi ya wazazi wanawaficha watoto hao manyumbani.

Bwana John Isiriri ni mmoja wa wazazi waliohudhuria kilele cha wiki ya elimu,amesema ni kweli kuna tatizo kwa watoto wenye ulemavu kwa kutopewa kipaombale tokea katika ngazi ya familia zao na hivyo kupelekea wengi wao kukosa elimu.

Pia amesema tatizo la ujauzito kwa watoto wa kike bado ni changamoto kwa watoto wao hasa wa sekondari, lakini wazazi sasa wanatakiwa kusimamia maadili ya watoto wao na pia kuchangia chakula mashuleni ili kupunguza vishawishi kwa watoto wa kike.

Maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu hufanyika kila mwaka na mwaka huu 2018 kimkoa yamefanyika katika wilaya ya Karatu kwa lengo la kuhamasisha utoaji wa elimu bora kwa shule za mkoa wa Arusha.