Viongozi wa Kata wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha
watakiwa kutafuta suluhu ya tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari.
Akitoa maagizo hayo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,mkuu
wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo katika kuhadhimisha siku ya kilele cha
wiki ya elimu Mkoani Arusha.
Amesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya elimu
Mkoani Arusha ni mimba kwa wanafunzi hasa wa Sekondari,ambapo kwa mwaka 2017
wanafunzi 237 waligundulika kuwa na ujauzito ikiwa wanafunzi 50 ni wa shule za
Msingi na 187 ni wa Sekondari.
Aidha,kuanzia Januari hadi Aprili 2018 jumla ya
wanafunzi 97 waligundulika kuwa na ujauzito ambapo wanafunzi 17 niwa shule za
Msingi na 80 wa Sekondari.
“Bado tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni
changamoto kubwa hasa wa sekondari,wazazi bado mna jukumu kubwa hasa la
kuhakikisha mnasimamia maadili ya watoto wenu na pia kuchangia fedha za chakula
mashuleni ilikupunguza vishawishi kwa wanafunzi hawa”.
Katibu Tawala msaidizi upande wa elimu bwana Gift
Kyando,amesema changamoto nyingine iliyopo katika sekta ya elimu Mkoani Arusha
ni baadhi ya watoto kutojua kusoma,kuhesabu na kuandika (KKK), kwa sababu
watoto hao hawapatiwi elimu ya awali kwanza kabla ya kujiunga na elimu ya
msingi.
Amesema mbali na changamoto hizo,elimu bure kwa Mkoa wa
Arusha imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya uwandikishaji wa
watoto darasa la kwanza.
Akisisitiza zaidi anasema mradi wa mpango wa kusaidia
kusoma,kuandika na kuhesabu (LANES) umeweza kusaidia sekta ya elimu kwa kiasi
kikubwa kwani mradi umeweza kuongeza Vitabu,Vifaa vya kufundishia na Vyombo vya
usafiri,ambapo kila halmashauri itapatiwa kopyuta 3 za kusaidia utunzaji wa
taarifa mbalimbali za wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment