Wednesday, July 12, 2017

KATIBU TAWALA,RICHARD KWITEGA ATEMBELEA KITUO CHA SOS CHILDREN VILLAGE

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, akiwa pamoja na baadhi ya vijana wanaolelewa katika kituo cha SOS Children Village tokea wakiwa na umri wa miaka 3 na baadhi ya walezi wao,Ngaramtoni.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu sana  na taasisi ya SOS Children Village kwenye shughuli wanazofanya hususani zakusaidia watoto wasio na wazazi.

Aliyasema hayo alipotembelea kituo hicho kwa lengo lakutaka kufahamu zaidi namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ilikuona nikwajinsi gani serikali inaweza kushirikiana nayo katika kuwalea watoto hao kwakuwa na wao niwatanzania wanahaki zote zakuhudumiwa na serikali yao.

“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hii katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa watoto wetu hawa na wao waweze kujisikia kweli serikali yao ipo pamoja nao.”

Aidha, amepongeza taasisi hiyo kwa kutoa malezi mazuri kwa watoto hao hasa kwakuwalea kama wapo na wazazi wao halisi hasa kwakuwapa elimu na huduma ya afya.

Bwana Kwitega amesisitiza zaidi kuwa serikali kwa kuanza inaweza kutoa ushirikiano kwa kuleta wataalamu wa elimu yani walimu na wataalamu wa afya ambao watakuwa waajiriwa wa serikali lakini wakitoa huduma katika kituo hicho.

Akitoa historia fupi ya taasisi hiyo,Mkurugenzi wa taasisi hiyo bwana Francis Msollo alisema kituo hicho kilianza mwaka 2000 kikiwa na nyumba 10 tu zakuishi watoto hao lakini mpaka sasa wamefikisha nyumba 15 na watoto 200.

Pia alisema mbali yakuwalewa watoto hao wasio na wazazi, taasisi inatoa pia msaada kwa wale watoto wenye mzazi mmoja kwakuwapa ufadhiri wa elimu inayotolewa katika taasisi hiyo.

Taasisi hiyo pia imetoa nafasi kwa watoto wanaozunguka maeneo ya taasisi hiyo kupata elimu inayotolewa katika kituo hicho.

Akisisitiza zaidi bwana Msollo alisema, Changamoto wanayokabilina nayo kwasasa nikwabaadhi ya wafadhili kujitoa katika kutoa fedha zakutoa huduma za afya na elimu na hivyo kuiomba serikali iangalie naoma yakusaidia taasisi hiyo ili watoto hao waendelee kupata elimu bora na afya.

Msollo amesema, mipango ya baadae ya taasisi hiyo nikuboresha mabweni ya watoto hao iliwaweze kuchukua watoto wengi zaidi wakiwemo watoto wa mbali na mazingira hayo, pia usafiri kwa watoto hao wanaotoka mbali huku elimu itolewe zaidi katika jamii juu yakuwahudumia watoto hao yatima katika maeneo yao.

Taasisi ya SOS Children Village iliaanzishwa mwaka 1984 huko Zanzibar na baadae kufungua vituo vingine vinne katika mikoa ya Mwanza,Dar es Salaam, Arusha na Iringa, hadi sasa imeshaeenea katika nchi mbalimbali kama South Afrika na Uganda.




Katibu Tawala Richard Kwitega, akimsikiliza mmoja wa vijana aliyelelewa na kituo cha SOS Children Village Bi. Anna Lomayani na sasa anafamilia yake.

Bwana Kwitega, akiwasalimia baadhi ya watoto wa shule ya awali wa kituo cha SOS Children Village.

0 comments:

Post a Comment