Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera,akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe za nane nane, katika viwanja vya maonyesho hayo,jijini Arusha. |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera amesema maonyesha
ya kilimo na mifugo, maarufu kama nane nane mwaka huu kwa kanda ya Kaskazini
yataongoza kwa ubora kwa nchi nzima.
Aliyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha maandalizi ya
sherehe hizo za nane nane kwa kanda ya Kaskazini ambayo yanajumuisha mikoa
mitatu ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.
Amesema kwa Serikali hii ya awamu ya tano niwajibu
wakila mtu kufanya kazi kwa bidii nakuacha kufanyakazi kwa mazoea, ili kila
mipango iliyowekwa katika maandalizi hayo yafanikiwe na kanda hii kushika
nafasi ya kwanza nakua mfano kwa nchi nzima.
Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
ameziagiza TANESCO na AUWSA kuhakikisha maji na umeme vinapatikana katika
maeneo husika ya viwanja vya maonyesho ya nane nane ndani ya wiki moja.
Pia, Gambo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Arusha kuunda tume yakufuatilia taratibu za matumizi
ya viwanja hivyo hasa katika wakati ambao sio wa maonyesho, ili kusaidia kupata
taarifa kamili itakayosaidia kutoa hali halisi kabla ya makabidhiano baina ya
taasisi iliyokuwa ikisimamia maonyesho hayo TASO na ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Arusha.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gelasius Byakanwa
amesema pia katika kikao kijacho nivizuri taarifa ya mapato na matumizi kwa
mwaka jana na mwaka huu isomwe kwa wajumbe ili waweze kupata hali halisi ya
mapato hayo.
Maonyesho ya nane mwaka huu yataratibiwa na ofisi za
makatibu tawala wa mikoa yote mitatu ya kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano na Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvivu na mpaka sasa ni makampuni 33 tu ndio yamedhibitisha ishiriki katika
maonyesho hayo, wananchi wote bado wanahamasishwa kushiriki kuanzia siku ya
mwanzo hadi mwisho.
Wakuu wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wakikagua maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha. |
Baadhi ya viongozi wa kutoka mikoa ya kanda ya Kaskazini waliohudhuria kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha. |
0 comments:
Post a Comment