Friday, July 28, 2017

TIMU YA RIADHA YA TAIFA YAAGWA RASMI MKOANI ARUSHA

Katinu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya riadha ya taifa, jijini Arusha.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akikabidhi fedha kwa kocha wa timu ya riadha ya Taifa alipokuwa akiiaga rasmi kwa ajiri ya safari ya London.



Timu ya riadha ya taifa imekabidhiwa kiasi cha shiling laki tano kutoka  ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kama mchango wakuiunga mkono timu hiyo na kuitakia kila la kheri katika mashindano ya dunia.

Akitoa zawadi hiyo katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema, mkoa umeguswa sana na juhudi zinazooneshwa na timu hiyo katika mashindano mbalimbali hivyo kupitia ofisi yake imetoa kiasi hicho ili kuwaunga mkono wanariadha hao.

“Ofisi ya mkoa imeona haitakuwa sahihi sana kuiacha timu hii iondoke hivi hivi bila yakuitakia kheri ya mafanikio katika mashindano hayo ya riadha ambayo niya dunia, wakati imeweka kambi mda wote katika mkoa huu”.

Amewahasa kuwa wanapotoka hapo wawe na mawazo ya ushindi tu na wakazingatie yale yote waliyofundishwa wakati wakiwa kambini na walimu wao.

Aidha, amewataka wanaobaki kambini waendelea na mazoezi kwa juhudi zaidi na wasife moyo kwani mashindano yoyote yanaitaji juhudi na nidhamu ya hali ya juu.

Akitoa salamu za shukrani mmoja wa washiriki wa timu ya taifa Alex Siumbu amesema anaamini wanaenda kushinda na si vinginevyo kwani wameweza kufanya mazoezi kwa mda mrefu na watanzingatia maelekezo yote waliyopewa na walimu wao.

Timu hiyo ya riadha yenye washiriki 8 inatarajiwa kuondoka jijini Arusha Julai 29 kuelekea Dar es Salaama kwa maandalizi yakuangwa kitaifa Julai 31 na kuanza safari yakuelekea London Uwingereza Agosti 1 kwenye mashindano ya dunia.

Baadhi ya wanariadha wa timu ya taifa ya riadha wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha( hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha za kuwaaga rasmi.

0 comments:

Post a Comment