Baadhi ya wadau wa maendeleo ya vijana waliohudhuria kikoa na serikali ya mkoa wa Arusha, wakisoma taarifa zakutoka serikalini. |
Taasisi binafsi zinashughulika na maendeleo ya vijana
jijini Arusha zimehaswa kuhakikisha zinashirikiana kwa kiasi kikubwa na
serikali katika kuweka wazi shughuli zao wanazofanya katika Mkoa wa Arusha.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana kwa mkoa wa Arusha,
kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa.
“Nafahamu kuwa taasisi hizi binafsi sio adui wa serikali
kilichopo ni kulikuwa na mahusiano ya mbali kati yenu na serikali, serikali
ilikuwa haitambui shughuli zenu na nyinyi mlikuwa hamfahamu serikali yenu inaitaji
nini”.
Gambo amesisizaidi kwa taasisi hizo kuhakikisha
zinafanya kazi ambazo ni hitaji kubwa kwa vijana wetu badala yakutekeleza
matakwa ya wafadhiri wao tu.
Amesema lengo kubwa lakukutanisha taasisi hizo na
serikali nikufahamiana na pia kuweka mikakati ambayo itaenda sambamba na
serikali ya awamu ya tano ambayo inapiga vita madawa ya kulevywa,mimba za utoto
na utegemezi.
Hivyo amezitaka taasisi hizo za maendeleo ya vijana
kuhakikisha zinatoa elimu yakutosha ya afya ya uzazi kwa vijana,madhara ya
madawa ya kulevywa na elimu ya ujasiliamali, ili vijana waweze kujikwamua
katika maisha kwakufanya kazi kwa bidii.
Aidha, amezitaka taasisi hizo kuzitambua fursa zilizopo
serikalini kama za mikopo kutoka mfuko wa taifa wa maendeleo ya vijana na asilimia
5 ya mapato kutoka katika kila halmashauri ambazo zinapelekwa kwa vijana.
Hivyo taasisi hizo zinatakiwa kuweka utaratibu
wakuisaidia serikali katika kuzisimamia fedha hizo ili ziweze kuwanufaisha
vijana kwa kiasi kikubwa na wao wakiendelea kuwapa mafunzo zaidi ya
ujasiliamali ikiwemo uwandikaji wa miradi mbalimbali.
Kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza kwa mkoa wa Arusha
kwa lengo lakufufua mahusiano ya karibu baina ya serikali na taasisi zinashughulika
na maendeleo ya vijana na moja ya makubalino waliyoafikiana nikuandaa kongamano
la vijana kimkoa na kamati mbalimbali zimeundwa zakusimamia muendelezo wa vikao
vijavyo.
0 comments:
Post a Comment