Katibu Tawala akitoa maelezo juu ya maadhimisho ya siku ya nane nane kwa kanda ya Kaskazini. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema kuwa maonyesho ya wakulima
maarufu kama nane nane ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja wa Themi
Njiro yataendelea kuwepo kama kawaida.
Ameyasema hayo baada yakutokea sitofahamu kwa wananchi kutokana
na iliyokuwa taasisi yakusimamia maonyesho hayo (TASO) kuzuiliwa kuendelea
kuratibu maonyesho hayo.
Aidha, amesema kwa mwaka huu maonyesho hayo yataratibiwa
kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Sekretarieti za Mikoa
ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara pamoja na TASO.
Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ikiwa ndio mwenyeji
wa maonyesho hayo ndio imepewa jukumu lakusimamia uwandaaji wa shughuli zote
katika viwanja hivyo.
Ametoa wito kwa washiriki wote wa maonyesho hayo kwa
mwaka huu 2017 kuanza maandalizi mapema
ikiwemo ulipaji wa ada ya ushiriki katika ofisi zilizokuwa za TASO ndani ya
viwanja vya nane nane ambapo kwa sasa kuna maafisa walioteuliwa kutoka katika
Wizara na Sekretarieti ya Mkoa kutumia ofisi hizo kwa shughuli hizo.
Pia shughuli nyingine za Maandalizi zikiwemo kuwasilisha
mahitaji ya idadi ya waoneshaji, Magari, na taarifa nyingine zifanyike katika
ofisi za TASO kabla ya Julai 20,2017.
Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo
“Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi
wa kati”,ambayo yataanza rasmi Agosti moja,2017 nakumalizika Agosti 10,2017.
0 comments:
Post a Comment