Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwasili wilayani Ngorongoro kuendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha. |
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiangalia moja ya bidhaa za kitamaduni zilizotengeneza na wakinama wa Eminyatta,wilayani Ngorongoro. |
Kassim Majaliwa akitoka katika moja ya nyumba za tamaduni za Eminyatta,katika kijiji cha Ololosokwani. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema sasa migogoro ya
ardhi nchini ifikie mwisho kwa viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri kutafutia
suluhu yakudumu katika maeneo yao.
Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akimwagiza mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuitisha kikao maalumu cha utatuzi wa mgogoro wa
ardhi uliopo katika kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro kati ya eneo la
hifadhi na makazi ya watu ambao umedumu kwa mda mrefu.
“Namuagiza Mkuu wa Mkoa akishirikiana na mkuu wa
wilaya ya Ngorongoro pamoja na kamati ya kijiji yakushughulikia migogoro ya
ardhi na wawekezaji wakae wajadiliane namna yakupata muafaka wa mgogoro huu’.
Amesema ni vizuri wananchi nao wakashirikishwa
pamoja na wawekezaji waliopo katika kijiji hicho ili maamuzi yatakayotolewa yawe
shirikishi kwa pande zote.
Hata hivyo amewapongeza wananchi wa Ololosokwani
kwakutambua umuhimu wakulinda na kuzithamini hifadhi za taifa na amewaadi kuwa
serikali yao ipo pamoja nao katika kuunga mkono utunzaji huo wa hifadhi.
Amesisitiza zaidi kwa wananchi kulinda amani ya nchi
yao kwa kuwatambua wageni wote wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu kusika
na pale wanapowatilia mashaka watoe taarifa katika mamlaka husika na mifugo ya
wenyeji ibainishwe haraka dhidi ya wageni.
Akifafanua ziadi Waziri wa maliasili na utalii
Jumanne Maghembe amesema nivizuri mifugo yote ya wanakijiji cha Ololosokwan
ikatambulika kwa kuwekewa alama ilikusaidia kubaini ile mifugo inayotoka nchi
jirani nakuingia kinyemela.
Amesema ongezeko la mifugo hasa yakutoka nje ndio
inayosababisha uvamizi wa maeneo ya hifadhi kwasababu wanakuwa wanatafuta
maeneo ya malisho.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema
tayari alishamuagiza mkuu wa wilaya ya Ngorongoro alipokuwa kwenye ziara yake
kuunda kamati ndogo itakayofuatilia mgogoro huo na tayari kamati hiyo
ilishaanza kazi ikiwa chini ya mkuu wa wilaya hiyo na ikimaliza kazi majibu
yatapelekwa kwa wananchi.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa waso,Loliondo. |
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amezipa miezi sita taasisi zisizo za kiserikali(NGO’s) zote za
wilayani Ngorongoro kuhakikisha zinabadili mfumo wake wa utendaji kwakufuati
usajiri.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa
halmashauri ya Ngorongoro na baadhi ya viongozi wa NGO’s katika ukumbi wa
halmashauri.
“Ninawapa miezi sita tu kwa NGO’s zote zilizopo
wilayani hapa kuhakikisha zanabadili mfumo wake wa utendaji kwa kufuata
shughuli walizosajiriwa nazo”.
Majaliwa amesema NGO’s nyingi hazifuati taratibu za
utendaji kulingana na shughuli walizojisajiri, nyingi zimekuwa zikipata fedha
kutoka kwa wafadhili na fedha hizo zinafanyiwa matumizi tofauti.
Pia amesema kuna baadhi yake zimefungua akaunti za
benki nje ya nchi na fedha zote wanazopata kutoka kwa wafadhili zinawekwa huko
wakati huo hazina akaunti yoyote kwa hapa nchini.
Majaliwa amesisitiza kuwa baada ya NGO’s zote
kukamilisha zoezi hilo atamtuma mkaguzi mkuu wa hesabu wa serikali kuja
wilayani Ngorongoro kukagua matumizi ya fedha zote zilizotumika tokea kila NGO
ilipoanzishwa na ikibainika kulikuwa na udanganyifu zitafutiwa usajiri wake
mala moja.
Hata hivyo Majaliwa ameshangazwa na wingi wa NGO’s
zilizopo wilayani Ngorongoro ambazo ni zaidi ya 30 wakati kuna mikoa mingine inaitaji
kuwa nazo lakini hakuna.
0 comments:
Post a Comment