Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa,akiwasalimia wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mkoa Mt. Meru. |
Waziri Mkuu Majaliwa azuru kabuli la merehemu Edward Moringe Sokoine, wilayani Monduli. |
Mhe.Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Emeirete wilayani Monduli. |
Kassim Majaliwa azindua wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Monduli. |
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Kassim Majaliwa amewataka watumishi wote wa serikali kuzingatia
uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.
Ameyasema hayo alipokuwa akuzungumza na watumishi wa
halmashauri ya wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada yakufungua wodi ya mama wajawazito
ya hospitali ya wilaya ya Monduli.
“Serikali ya awamu ya tano niyawawajibikaji,waadilifu
katika sekta za umma”,alisema Majaliwa.
Amewataka watumishi wawasikilize,wawahudumie na
kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina yoyote ile.
Hii itasaidia kuonyesha matokea bora ya kila
mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi zaidi
serikalini.
Aidha amewataka viongozi wa halmashauri kusimamia
fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na zikafanye shughuli
ambazo zilipangiwa.
Kila sekta katika halmashauri ihakikishe inapanga
majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa mto wa Mbu wilayani Monduli. |
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ha Muungano wa
Tanzania,Kassim Majaliwa amekonga nyoyo za wakazi wa Monduli kwakuwakabidhi
hati ya shamba la Manyara Ranch yenye jina la halmashauri ya Monduli.
Akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri ya Monduli Steven Ulaya
amesema shamba hilo lilikuwa kilio cha mda mrefu kwa wakazi wa Monduli hususani
wanakijiji cha Isilarei na Olutukai.
Ambao ndio wamiliki halali wa shamba hilo chini ya
halmashauri ya Monduli lakini lilimilikishwa kwa taasisi ya TCLT (Tanzania Land
Conservation Trust) kimakosa.
“Nawakabidhi hati hii ya shamba yenye jina la
halmashauri kama msimamizi wa shamba hili kwaniaba ya wananchi wa vijiji vya
Isilarei na Olutukai”.
Shamba hili lilikuwa linamilikiwa na taasisi ya TCLT
kwaniaba ya halmashauri lakini serikali ya Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa Mkoa
wake Mrisho Mashaka Gambo aliagiza halmashauri ya wilaya ya Monduli kuhakikisha
hati hiyo inarudishwa chini ya halmashauri.
Ndani ya wiki moja tayari halmashauri ikawa imefanya
maamuzi yakubadili kwakufuata taratibu zote zakubadili jina la umiliki kutoka
TCLT nakusomeka halmashauri ya wilaya ya Monduli amboa ndio wamiliki halali wa
shamba hilo.
Shamba hilo sasa lipo chini ya halmashauri ya wilaya
ya Monduli na wanakijiji wa vijiji hivyo wanaruhusiwa kutumia ardhi hiyo
kwakufuata taratibu kwa shughuli za maendeleo yao.
Mheshimiwa Majaliwa alikuwa na ziara ya siku moja
katika wilaya ya Monduli na ataendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha kwenye wilaya ya Karatu na kisha Ngorongoro.
0 comments:
Post a Comment