Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha. |
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta
mbalimbali hasa za viwanda hapa nchini.
Aliyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa
jiji la Arusha nakuwashauri wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa
kwakuanzisha viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali
ilivyo.
“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na
niruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.
Hata hivyo amewata waendelee kushirikiana na serikali yao ya awamu ya tano
kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini
ili wawe na amani na waweze kuwekeza zaidi.
Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi
kwenye sekta binafsi hasa kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka
usawa katika biashara na kukuza ushindaji wa biashara.
Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali
kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi ya rasilimali za ndani napia kuzipunguzia
ushuru ili viwanda viweze kukuwa kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga
nchi ya viwanda.
Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi
katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(Kulia) na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laiza, katika mkutano na wafanyabaishara wa jiji la Arusha. |
0 comments:
Post a Comment