Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisoma mabango ya wananchi wa kijiji cha Qandged wilayani Karatu baada yakufunga njia kuzuia msafara wake usipite. |
Kassim Majaliwa akikagua mfereji wa maji uliojengwa na World Vision unaopeleka maji kwenye kisima katika kijiji cha Jobaj. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa
Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kuondoa mashine zakupampu maji zilizowekwa
kwenye chanzo cha maji cha kijiji cha Qangded kata ya Eyasi wilayani Karatu.
Akitoa maelekezo hayo Majaliwa wakati alipokuwa anaongea na wanakijiji wa Jobaj
katika mkutano wa hadhara ambapo alizindua kisima cha maji.
Alisema mashine hizo zimekuwa zikitumika kunyeshea mashamba ya wafanyabiashara wakubwa wa vitunguu na mahindi nakusababisha kasi ya maji kwenye mifereji kupungua nakupelekea wakazi wengi wa kijiji hicho kukosa maji kwa mda mrefu.
“Baada ya siku moja Mkuu wa wilaya apite kukagua na
akikuta bado mashine hizo zipo azikamate nakuwachukulia hatua kali wahusika
kwakuwa wanaharibu vyanzo vya maji”. Alisema.
Pia amewataka wananchi wote kuwa walinzi wa vyanzo
vya maji vilivyopo katika maeneo yao na watoe taarifa mapema kwa mamlaka husika
pale wanapogundua kuna uharibifu umefanyika.
Wananchi wanatakiwa kufuata sheria yakutofanya
shughuli zozote za uzalishaji ndani ya mita 500 kutoka katika vyanzo vya maji
na waliofanya hivyo waondolewe mara moja.
Majaliwa amelipongeza shirika la World Vision Karatu
kwakujenga mifereji yakutoa maji kwenye chanzo cha maji hadi kwenye visima ambavyo wananchi
wanapata maji,hizo ni juhudi kubwa zilizofanywa na shirika hilo na serikali
inatambua mchango wao huo mkubwa.
Amewata mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri kujenga utamaduni wakusiliza kero mbalimbali za wananchi
nakuzichukulia hatua mara moja.
Waziri Mkuu Majaliwa akiangalia naoma maji yanavyokusanywa kwenye mrefeji kabla yakuelekezwa kwenda kwenye kisima cha kijiji cha Jobaj |
Majaliwa akikagua moja ya shamba lililolimwa kutokana na kilimo cha umwagiliaji cha kijiji cha Qandged wilayani Karatu. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia kwake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakikata utepe kama ishara yauzinduzi wa kisima cha maji cha kijiji cha Jobaj wilayani Karatu. |
Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa(MB) akuzungumza na wananchi wa Karatu katika uwanja wa Baraa Karatu Mjini baada yakumaliza ziara wilayani humo. |
0 comments:
Post a Comment