Amewasihi sana wazazi ambao bado wanaendela kuwaficha watoto kama hao waache mara moja kwani hata wao bado wana fursa kubwa katika jamii yetu,hivyo wanatakiwa kupewa nafasi kama ilivyo kwa watoto wengine.
Aidha, amezitaka halmashauri zote za mkoa wa Arusha
kuhakikisha zinatenga bajeti maalumu yakuendesha michezo kwa watoto wenye
ulemavu kama ilivyo kwa watoto wengine na kuhakikisha zinashiriki katika
mashindao yajayo.
Serikali inatambua vizuri sana mahitaji ya kundi hili la
watoto wenye mahitaji maalumu ndio maana ikatenga bajeti yakutosha mashuleni
ili waweze kupata chakula chakutosha asubuhi na mchana.
Emmanuel Maundo akikabidhi cheti cha chukrani kwa bwana,Yuzra Mushree kutoka Kampuni ya A and B Limited,waliotoa mchango wao mkubwa katika kufanikisha safari ya timu ya walemavu wa Akili. |
Akiongezea zaidi,amesema ofisi ya mkuu wa Mkoa Arusha
itaendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo nakutoa ushirikiano kila mara ili
kuwasaidia watoto hao waweze kuendelea na michezo yao.
Pia mratibu wa SOT Bwana Antony Mushi, amesema timu ya
watoto hao walemavu wa akili imeweza kuibuka na medari 6 za Dhahabu,12 za Fedha
na 14 za Shaba nakufanikiwa kutoa watoto watatu ambao watashiriki mashindano
yakimataifa yatakayofanyika Machi 2019,huko Abu Dhabi Uarabuni.
Amewashukuru wafadhili mbalimbali waliojitokeza katika
kusaidia mahitaji mbalimbali ya timu hiyo hususani tiketi za mabasi kwenda
Zanzabar na kurudi,vyakula na vifaa vya michezo.Amehimiza wasichoke kusaidia
kwani bado uhitaji nimkubwa na kuomba na wafadhili wengine wajitokeze zaidi.
Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Onoka, nae amesema kama mkoa atahakikisha mashindao hayo ya watoto wenye ulemevu wa akili yanafanyika kila mwaka kwa Mkoa wa Arusha.
Afisa Michezo Mkoa wa Arusha Mwamvuta Onoka akimvisha medali mmoja wa watoto wenye ulemeavu wa akili walioshiriki mashinda ya michezo mbalimbali,Zanzibar. |
Amesema michezo kwa watoto hao nimuhimu sana kwa afya
zao hivyo hamna budi kuyafanya kila mwaka badala yakusubiri kila baada ya miaka
3 au 4.
Olimpiki maalumu kwa Mkoa wa Arusha ilianza mwaka 1990
kwa mashindano hayo kufanyika hapa hapa Arusha na baadae yaliendelea katika
mikoa mingine nchini.
Emmanuel Maundo akimvisha medali mmoja wa watoto walioshiriki mashindano ya Olimpiki Maalumu,Zanzibar. |
0 comments:
Post a Comment