Muheshimiwa Jenista Muhagama,Muheshimiwa Antony Mavunde na Muheshimiwa Mrisho Gambo wakikabidhi mfano wa Hundi ya Milioni 120 kwa akinamama 600,Jijini Arusha. |
Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao
kwa kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za
maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika
familia zao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira
na wenye Ulemavu Jenista Muhagama alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya
mkopo wa akinamama wajasiliamali, Jiji la Arusha.
Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka
kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za
familia na jamii kwa ujumla.
“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata
tunda la embe katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo
hiyo kwa mara nyingine”.alisema
Aidha,amewahasa wakatumie vizuri mikopo hiyo na waache kwenda kununua vitu
ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na familia zao.
Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha
matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake
kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya
chama cha mapinduzi.
Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote
watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya
riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.
Pamoja na akimama kipatiwa hiyo mikopo wanaweza pia kutafuta
fursa kubwa zaidi katika miradi mikubwa inayofanywa na serikali,ili na wao
waweze kukua katika biashara zao.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa juhudi
alizozifanya za kusaida makundi maalumu ya vijana,wanawake na wenye ulemevu
katika kuwatengenezea ajira zaidi ya 200.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema akinamama ni
kundi kubwa sana linalotegemewa kwa asilimia kubwa katika ngazi za familia na
jamii kwa ujumla,hivyo aliona hana budi kutafuta namna yakuwawezesha ili waweze
kujikwamua katika maisha yao.
Amewataka wenye mapenzi mema waendelee kusaidia
akinamama katika Nyanja ya kujikwamua kiuchumi ile pale wanapokosa usaidizi
basi waweze kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao na wategemezi wao.
Akisisitiza zaidi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel
Daqarro,amesema mwanamke nisawa na hewa ya oxjeni pale inapokosekana inaleta
maafa makubwa na pengine kupoteza kabisa uhai wa binadamu.
Akitoa salamu za pongezi
Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo kama
mmoja wa wadau amesema alichofanya Gambo ni jambo la kuigwa na watu wengine na yeye
atachangia kiasi cha milioni 20 ili wakimama wengine 100 waweze kukopeshwa.
Mikopo isiyokuwa na riba ya kuwezesha makundi mbalimbali katika Mkoa wa Arusha ilianza kwa vijana 200 kukopeshwa pikipiki na baada ya kufanya marejesho yao kiasi cha milioni 120 kimetolewa kuwakopesha akinamama 600 kama mtaji wakufanya biashara mbalimbali.
Baadhi ya Wadau na akinamama walioudhuria sherehe za kuwakabidhi mikopo akinamama 600 wa Jiji la Arusha. |
0 comments:
Post a Comment