Friday, March 23, 2018

Madini ya Vito Kuongezewa Thamani

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisikiliza maelezo ya namna yakung'arisha madini kutoka kwa Mkufunzi Bi.Mariam Swalehe wa kituo cha kuongeza thamani Madini aina ya Vito,Jijini Arusha.


Kituo cha kuongeza thamani ya madini (Tanzania Geological Centre),kimejipanga kutoa mafunza kwa wingi kwa wajasiliamali  ya namna yakuongeza thamani ya madini ya Vito.
Akitoa pongezi kwa kituo hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema niwakati sasa kwa watanzania kujivunia na kunufaika na madini yao.
Amesema kituo hicho kimefanya vizuri sana kuanzisha mafuzo hayo kwa wajasiliamali ili kuwaongezea ujuzi wa utambuzi  wa madini ya vito na hii itasaidia kupunguza udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu.
“Mafunzo haya mnayotoa yatasaidia kupunguza udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa  madini kwa kutengeneza madini feki nakuwauzia wateja wao.”alisema
Amemshauri mratibu wa kituo cha kuongeza thamani kuanza kufikiria namna ya kuwa na chapa za Tanzania katika madini ili kujitangaza zaidi ndani na nje ya nchi kuliko kutokuwa nayo hii inapelekea nchi nyingine kupata jina katika soko kwa kutumia madini yetu.
Aidha,amesema ameshafanya mawasiliano na balozi wa India kuwaomba kuwafadhiri baadhi ya wataalamu kwenda India kupata mafunzo zaidi ya namna yakutambua na kuyaongezea thamani madini na balozi amesharidhia.
Gambo ameshauri pia wadau wa madini nao wangeshirikishwa juu yakudhamini baadhi ya wajasiliamali kupata elimu hiyo na hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wajasiliamali watakaopa elimu hiyo.
Pia,Mratibu wa kituo hicho bwana Erick Mpesa amesema,kituo hicho kilianzishwa 2014 na mpaka sasa tayari wanafunzi 300 wameshahitimu mafunzo hayo.
Amesema bado wanaendelea na juhudi za kuandaa makumbusho itakayotumika kutunza madini yote yanayopatikana hapa nchini,hii itasaidia hata kama madini yetu yataisha lakini kumbukumbu inatakiwa kuwepo kwa vizazi vijavyo.
Mkuu wa mkoa yupo katika ziara ya kutembelea viwanda vya Arusha kwa siku 3 na lengo ni kusikiliza changamoto zinazowakabiri wawekezaji kwa kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano nikuhakikisha nchi inaingia katika hatua ya viwanda.




Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Kuongeza Thamani Madini Bwana Erick Mpesa akimwelezea juu ya utambuzi wa madini unavyofanywa na kituo hicho, pembeni yake ni Mkurugenzi wa madini Bwana Adamu,Jijini Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akimsikiliza Mkufunzi Peter John akimwelezea namna wanavyochonga bidhaa kwa kutumia mawe,Jijini Arusha.


Katibu Tawala Mkoa Richard Kwitega,akikagua moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Sunkist,Jijini Arusha.


0 comments:

Post a Comment