Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba,akimkabidhi bwana Peter Urio kadi ya Pikipiki,Mkoani Arusha. |
Akitoa kauli hiyo,Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa
Mwigulu Nchemba katika kikao chake na waendesha bodaboda wa mkoa wa Arusha
alipokuwa akiwagawia kadi za umili wa bodaboda kwa madereva 107 waliofanikiwa kumaliza mkopo
wa mradi wakukopesha pikipiki ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kauli hiyo imetolewa na mheshimiwa waziri baada ya Mkuu
wa Mkoa wa Arusha kutoa ombi maalum kwake lakuwaruhusu madereva bodaboda hao
kujifunza sheria kwanza kisha ndio polisi waanze utaratibu wakuwakamata wale
wote watakaokuwa wamekiuka sheria za barabarani.
Mwigulu Nchemba amewasihi bodaboda wote nchini
kuchukulia hii kazi kama yenye heshima ili iweze kuwabadilisha maisha yao na
tegemeze wao.
Aidha,amesisitiza utoaji wa leseni kwa bodaboda
utazingatia kwa wale ambao watakuwa wanamiliki kofia mbele na hata akiwa na
cheti pia atapatiwa leseni,pia abiria atakaekaidi kuvaa kofia basi atapatiwa
adhabu yeye nasio dereva kama ilivyokuwa awali.
Akichangia zaidi juu ya mradi huu,Mwiguli Nchemba
atachangia kiasi cha shilingi milioni 10 ilikusaidia vijana wengine waweze
kukopeshwa pikipiki kwa wingi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewaambia
bodaboda kuwa wanaweza kutumika katika kubeba watalii ikiwa tu wataweza kufuata
sheria na taratibu za barabarani.
Amewapongeza watendaji kata na maafisa tarafa wa Jiji la
Arusha kwakuonyesha ushirkiano mkubwa katika kufanikisha makusanyo na kwa
wakati, na kiasi cha shilingi milioni 306 tayari zimesharudishwa na milioni 200
zitatumika kukopesha wamama wajasiriamali wadogo kwa mkopo wa shilingi laki 2
kwa wamama 500.
Amesema kiasi cha pesa kinachobaki cha zaidi ya milioni
100 kitatumika kukopesha waendesha bodaboda wengine,hii itasaidia kuwawezesha
vijana wengi kumuliki pikipiki zao wenyewe badala yakutegemea pikipiki za watu
wengine ambazo zinawabana sana.
Kamanda wa polisi kitengo cha barabarani Joseph
Buberwa,amewataka bodaboda kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti,wapunguze
spidi barabarani hususani kwenye makazi ya watu.
Amesema kuwa polisi barabarani hawatawakamata bodaboda
ambao hawana leseni lakini wana cheti cha udereva na watawapa mda wakuhakikisha
wanapata lesenina amewapongeza madereva 250 waliofanikiwa kuhitimu mafunzo ya
udereva.
Akisisitiza zaidi mwenyekiti waumoja wa madereva
bodaboda (UBOJA) bwana Mauridi Makongoro,amesema mradi huo umewanufaisha sana
bodaboda wengi kwani umewatoa katika mazingira yakuendesha bodaboda za watu
wengine na sasa wanamiliki zao wenyewe na wameweza kuingiza kipato chakutosha.
Mradi huu ulianzishwa mwaka 2017 na mheshimiwa Gambo kwa
lengo lakuwakwamua bodaboda wa Jiji la Arusha katika changamoto yakukosa mtaji
wakumiliki pikipiki zao, vijana 200
walifanikiwa kukopeshwa pikipiki hizo na kati yao 107 wamemaliza mkopo
nakukabidhiwakadi za umiliki wa pikipiki na wengine wanaendelea na marejesho.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba,akiwa kwenye picha ya pamoja,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,viongozi wa CCM Wilaya ya Arusha na bodaboda wa Jiji la Arusha. |
Baadhi ya waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mwigulu Nchemba(hayupo pichani) kwenye kikao chakukabidhi kadi za umiliki wa bodaboda,Jijini Arusha. |
0 comments:
Post a Comment