Saturday, July 28, 2018

MIRADI MINGI YA MAJI HAINA UHALISIA WA THAMANI

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji  Mhe. Stella Manyanya (MB), akipanda mtu kama ishara ya uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya bodi ya Wahandisi tangu kuanzishwa, pembeni yake ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo jijini  Arusha.


Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) amewaagiza mafundi Sanifu kufanya kazi kwa uwaminifu kwa simamia miradi vizuri.
Ameyasema hayo alipofungua kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya bodi ya wahandisi nchini katika ukumbi wa Arusha Tekiniko (Arusha Tech), jijini Arusha.
“Miradi mingi ya halmashauri hasa ya maji haina uhalisia wa gharama zake na wasimamizi wakuu ni nyinyi mafundi Sanifu, niwakati sasa umefika mkafanye kazi zenu kwa uwaminifu”.
Aidha, ameiagiza bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuhakikisha inatoa mikopo kwa mafundi sanifu ilikuongeza idadi yao kwani kwasasa wapo 927 ni wachache sana kulingana na mahitaji ya nchi.
Serikali inawathamini na kutambua mchango unaotolewa na mafundi sanifu katika kujenga uchumi wa viwanda, hivyo tumuunge mkono rais wetu kwa juhudi zake anazozionyesha.
Mafundi Sanifu,Mchundo na wahandisi ndio watakaoisaidia serikali kufanikisha ujenzi wa viwanda na kuifanya nchi yetu kuingia katika uchumi wa kati wa viwanda.
Bodi ya wahandisi imefanya kongamano lake kwa mala ya kwanza na hii ni moja yakuadhimisha miaka 50 ya bodi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1968 na maadhimisho yatafanyika Dodoma Septemba 5-7,2018.


Baadhi wa Wahandisi wakimsikilia mgeni rasmi, waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Eng.Stella Manyanya( hayupo pichani) katika  kongamano la miaka 50 ya bodi ya wahandisi,Jijini Arusha.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Eng. Stella Manyanya akihutubia katika kongamano la wahandisi lililofanyika jijini Arusha.


0 comments:

Post a Comment