Shule
ya Sekondari Kisimiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mkoani Arusha
imefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita kwa kushika
nafasi ya pili kitaifa kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo, huku
shule ya Sekondari Kibaha ikishika nafasi ya kwanza na shule ya Sekondari
Kemebos ikishika nafasi ya tatu,hii ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na
baraza la mitihani Taifa.
Aidha
matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri ni mwendelezo wa historia ya
kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita kwani kwa
miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa ,ambapo mwaka
2016 ilishika nafasi ya kwanza,mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka
huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa kwa watahiniwa wake 67 kupata daraja
la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata
daraja la pili.
Nuru
ya shule hii ya Sekondari Kisimiri yazidi kuangaza kwenye Mkoa wa Arusha wenye
shule 17 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na Binafsi 14.Shule zenye
watahiniwa chini ya 30 kwa mkoa wa Arusha zipo 13 ikiwa shule 1 tuni ya
serikali na 12 ni binafsi.
Ufahuru
huu umepelekea Mkoa wa Arusha kupata shule nyingi zilizofanya vizuri katika
mtihani wa kidato cha sita,mbali na Kisimiri shule nyingine 10 zilizofanya
vizuri zenye watahiniwa zaidi ya 30
ni;Iluboru,Embarway,Mlangarini,Gawako,Loliondo,Engutoto,Irikisongo,Maji ya
chai,Nainokanoka.Shule iliyofanya vizuri yenye watahiniwa chini ya 30 ni
Mwandet.
Hata
hivyo baadhi ya shule katika Mkoa wa
Arusha zinatakiwa kuongeza juhudi katika kuinua kiwango cha ufauru nazo ni;
shule ya sekondari Florian na Makiba.
0 comments:
Post a Comment