Ameyasema hayo alipokuwa akuzunguza na wajasilimali
wautalii wa utamaduni katika soko la Masai,jiji Arusha.Amesema bidhaa za utalii
wa utamaduni ni nembo tosha yakutangaza nchi yetu.
“Ni kweli kuna Changamoto katika ujasiliamali huu wa
utalii wa utamaduni hususani kwenye tozo mbalimbali mnazotozwa na mamlaka
husua.”
Serikali ipo tayari kwenye mchakato wakutatua Changamoto
hii ya tozo na kuona ni namna gani soko la vinyago nchini Tanzania linakuwa na
kujulikana zaidi kimataifa, kuliko kwa sasa soko kuu linajulikana lipo jijini
Nairobi wakati wazalishaji wakubwa ni watanzania.
Dokta Mwakyembe alikuwa kwenye ziara ya siku 3 Mkoani
Arusha,ambapo ameweza kufungua redio mpya ya kijamii (TBC FM),aliweza
kutembelea kituo cha redio cha Sunrise,alifungua mkutano wa maafisa habari na
mawasilino serikali,ameweza kukutana na wadau wa utamaduni,sanaa na michezo na
ameweza kutembelea soko la vinyago la jijini Arusha.
Waziri Mwakyembe akizungumza na baadhi ya watalii waliofika katika soko la vinyago,jijini Arusha. |
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe akitazama moja ya bidhaa zinazopatikana katika soko la vinyago jijini Arusha. |
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe, akipokea zawadi ya kikombe kilichotengenezwa kwa shanga kwa mmoja wa wajasiliamali wa soko la vinyago jijini Arusha. |
0 comments:
Post a Comment