Mkuu wa
Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti na mabati
500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru Sakina.
Msaada
huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na viongozi
mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Arusha.
Akipokea
msaada huo,Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati 100
kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa na ongezeko
kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru wanaotoka maeneo hayo
hivyo ujenzi huo utasaidia kupunguza wagonjwa
katika hospitali hiyo.
Pia
yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa bweni la
shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza kila kitu.
“Napenda
kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure Sakina
na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa tumeshaanza mkakati wa ujenzi wa madara kwa shule za
msingi na Sekondari,hivyo nitagawa hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge
Zahanati kata ya Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni
lililoungua”.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV
Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja
ya shughuli zao zakusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Tumetoa
mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika kusaidia
jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.
Aidha
Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema kutokana na wingi wa wananchi waliopo katika
kata ya Murieti Zahanati hiyo itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi
miezi 2 Zahanati hiyo itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.
Ukosefu
wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa Mkoa Gambo
kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa
wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.
|
0 comments:
Post a Comment