Wednesday, October 5, 2016

GAMBO ACHANGIA MABATI 200


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo achangia mabati 200 kwaajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha kijiji cha Engaresoro.
 Kutokana na changamoto nyingi zinazoikumba  sekta ya afya hususani  kwenye Zahanati na Vituo vya afya mbalimbali hapa nchini ndio vinapelekea kuwa na huduma duni za kiafya.
“Mimi nitachangia mabati 200 kwaajili ya ujenzi wa chumba hicho cha upasuaji na ninaomba wananchi mjitokeze kwa wingi katika ujenzi wa chumba hicho ili tuweze kunusulu maisha ya kinamama na watoto wanaozaliwa”.
Ukosefu wa vitendea kazi,upungufu wa watumishi wa afya na ukosefu wa chumba chakujifungulia ndio changamoto zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha Engaresero Wilayani Ngorongoro.
Akitoa malalamiko hayo Bi.Omega Lemra alisema wakinamama wengi wanapata shida sana wanapoenda kujifungua katika kituo cha afya cha Engaresero kwasababu hakuna chumba cha upasuaji kwa wale wamama wanaojifungua kwa upasuaji.
“Tumekuwa tukipata sana shida wakinamama ambao tunaitaji kujifungua kwa upasuaji kwenye kituo chetu cha afya kwasababu hakuna chumba cha upasuaji na hivyo kutulazimu kwenda Wilaya ya karibu ya Karatu ambapo pia kuna umbali”,alisema Omega.
Aidha Gambo amewasisikitiza wananchi wa Engaresero kuchangia  mfuko wa bima ya afya(CHF) ilizipatikane fedha kwaajili yakununua vifaa tiba katika kituo hicho cha afya.
Akifafanua zaidi juu ya upungufu wa watumishi wa afya Mganga Mkuu wa Mkoa,Dokta Frida Mokiti,alisema halmashauri ya Ngorongoro ipeleke maombi ya watumishi wa afya wanaoitajika katika kituo hicho nakuwaweka katika bajeti ili waweze kuajiriwa mapema iwezekanavyo.
Muheshiwa Gambo yupo katika ziara Wilayani  Ngorongoro,ambapo anakutana na wananchi wa vijiji mbalimbali nakusikiliza matatizo huku mangine yakipatiwa ufumbuzi na mengine yakichukuliwa kwaufuatiliaji zaidi.



Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Engaresero,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo(hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao katika ziara yake kwenye kijiji hicho, Wilayani Ngorongoro.

0 comments:

Post a Comment