Rais
Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate
uhuru na tangu atimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro
barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya hiyo ianzishwe.
Haya
yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38
cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.
Gambo
alisema barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami na itaunganisha mji wa Wasso hadi Sale
kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.
Gambo
ameeleza katika Kikao hicho kwamba Rais Magufuli ameagiza kuanza
kujengwa kwa barabara hiyo mara moja kwa kiwango cha lami kama
alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.
Amesema
barabara hiyo inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha
( TANROADS).
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya
Ngorongoro ,Wilaya haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia alisema fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya
dunia sio msaada bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo
Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.
Akitoa
shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa
mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa
furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.
Wilaya
ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha ambapo Wilaya hii
inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za
uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na
kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.
Hivi
sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya za
Mkoa wa Arusha zikiwemo barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja
wa Mkoa Mhandisi John Kalupale.
Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha wakisikiliza agenda mbalimbali zikijadiliwa za kikao cha 38 cha bodi hiyo. |
0 comments:
Post a Comment