Wednesday, October 26, 2016

GAMBO ASHIRIKI UJENZU WA DARAJA FUPI



Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo ameshiriki ujenzi wa daraja fupi(drift) katika kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara na tarafa ya Engarenaibow kwa lengo lakuhamasisha wananchi na viongozi wengine.

Akitoa msisitizo kwa viongozi kujitoa sana pale wanapoitajika kushiriki shughuli mbalimbali za  maendeleo kwa wananchi wao hasa zile ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe.

“Viongozi mbalimbali wasiwe wazito kujitoa katika shughuli kama hizi za maendeleo ya wananchi na hasa ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe nivema basi na serikali nayo kupitia viongozi kwa ngazi tofauti kujitokeza nakuunga mkono”.

Mradi huo wa daraja fupi(drift) ulianza rasmi mnamo Octoba ,2016 kwa lengo lakuunganisha vijiji viwili vya Orgirah na Igulailungwa ambavyo vilitenganishwa kwa ukosefu wa daraja hilo fupi na kupelekea kwa vijiji hivyo kukosa mawasiliano.

Aidha mradi huo mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 9 ambapo mpaka sasa ni milioni 6 tu ndio zimetumika katika ujenzi huo, ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia 450,000, Mkurugenzi wa halmashauri alichangia 640,000 na nguvu za wananchi ni milioni 5.

Hata hivyo Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa juhudi walizozianza za ujenzi huo na hivyo serikali itawasaidia pale penye mapungufu na wananchi wenyewe wanatakiwa kujitokeza zaidi hususani kwenye shughuli kama hizo za maendeleo.

Mradi huo bado unamapungufu ya shilingi milioni 2 ili kukamilisha milioni 9 kama gharama nzima ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa aliaidi kuchangia mifuko 30 ya simenti,pesa taslimu 500,00 na kutoa katapila ikiwa wananchi watakuwa tayari kuchangia mafuta. 
Meneja wa TANROAD Arusha Enginia John Kalupale aliaidi kuchangia mifuko 50 ya simenti.

Pia mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Lekule Ole Laiza atachangia mifuko 30 ya simenti, mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido bwana Sabore Molleiment atachangia 500, 000, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido  Juma Muhina nae atachangia 400,000 na Halmashauri yenyewe itaenda kujadili kwenye vikao vyake namna yakusaidia ujenzi huo.

Gambo bado yupo ziarani Longido huku akishirikiana na wananchi wa Wilaya hio katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao.


Wananchi wa kijiji cha Orgirah wakishiriki katika ujenzu wa daraja fupi(drift) kwenye kijiji chao.

Hili ndilo daraja fupi(drift) lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara Wilayani Longido.

0 comments:

Post a Comment