Tuesday, October 25, 2016

Mtendaji wa Kata awekwa chini ya ulinzi wa polisi



Mkurugenzi halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi  mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari  Natroni Flamingo.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo  milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya wananchi.

Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya fedha zilizotajwa  kwenye taarifa hiyo.

Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua Bi.  Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.

Pia fedha hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200 ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.

Hivyo kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya ubadhilifu huo.

Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo yupo katika ziara ya kikazi Wilayani Longido kwa mda wa siku 5 ilikujionea maendeleo na pia kusiliza Changamoto mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.

 

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Meligoi walioikata taarifa ya mtendaji wa kata yao, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara, kijiji hapo.

0 comments:

Post a Comment