Saturday, April 7, 2018

Rais Magufuli Afungua Kituo Cha Utalii Cha Polisi

Rais John Pombe Magufuli akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kituo cha polisi cha Utalii,kulia kwake ni Ispecta Simon Sirro (Mkuu wa Polisi) na kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba,jijini Arusha.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, ametoa Bilioni 10 kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba za polisi wa vyeo vya chini nchi nzima.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na jeshi la polisi la mkoa wa Arusha katika sherehe za kuzindua  ofisi ya kidiplomasia ya utalii,Nyumba za makazi ya polisi na vituo 2 vya polisi wilayani Arusha.
Amesema kutokana na juhudi zilizofanywa na mkoa wa Arusha wa kujenga nyumba za polisi 31 baada ya nyumba 13 kuungua na moto mnamo Septemba 2017 na kusababisha familia 14 kukosa makazi.
Amewataka wakuu wa Mikoa wengine nchini kuiga mfano huo wa kujenga nyumba za polisi kwa  kuwashirikisha wadau mbalimbali kwani zilizoungua ni 13 na zimejengwa 31 zaidi ya zilizoungua.
Hata hivyo amewashauri pia wabunge watumie kiasi cha fedha cha mfuko wa jimbo katika kusaidia kujenga nyumba za polisi katika majimbo yao badala ya kuwaachia wakuu wa mikoa peke yao.

Rais Magufuli akizindua nyumba za makazi ya polisi ya Naura,akiwa na waziri Mwigulu Nchemba na Ispecta Simon Sirro, jijini Arusha.

Aidha, Magufuli ametoa ajira 1500 ya wahitimu wa jeshi la kujenga Taifa(JKT) kuajiriwa katika jeshi la polisi, ili kuongeza nguvu zaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda usalama.
Amelitaka jeshi la polisi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani amefurahishwa na maonyesha yaliyoonyeshwa katika sherehe hizo ambayo yametoa picha nzuri kwa nchi kuwa jeshi la polisi lipo imara na yeye ataendelea kuwaunga mkono kwa kila watachoamua kufanya.
Magufuri amelitaka jeshi la polisi nchini kurekebisha mapungufu madogo madogo yaliyojitokeza katika jesho hilo yakiwepo ya rushwa na uonevu kwa wananchi ambayo yamekuwa yakichafua jina la jesho hilo kwani yanafanywa na baadhi ya polisi.

Rais John Pombe Magufuli akiteta jambo na mkuu wa Polisi Ispecta Simon Sirro katika sherehe ya uzinduzi wa kituo cha utalii cha polisi,jijini Arusha.

Akisoma taarifa fupi ya ujenzi Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amesema ujenzi wa kituo cha polisi cha kidiplomasi kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 193 ambapo ni michango kutoka kwa wadau na serikali.
Aidha, katika ujenzi wa kituo cha polisi cha Murieti kimegharimu kiasi cha milioni 260 na ujenzi wa nyumba za polisi 31 zimegharimu kiasi cha milioni 550 ambapo milioni 250 zimetoka serikalini,milioni 50 zimetolewa na polisi na wadau mbalimbali wamechangia kiasi cha milioni 250.
Amesema jeshi la polisi nchini limeendelea kulinda usalama wa raia na mali zao na hivyo kupelekea kupunguza matukio ya uharifu kwa kiasi kikubwa na hata pia kudhibiti ajari za barabara kwa kiwango kikubwa.

Kikosi cha kuzuia uwarifu cha jijini Arusha kikionyesha moja ya maonyesho yake mbele ya Rais Magufuli (hayupo pichani)  katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya polisi, Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru Rais kwa juhudi zake alizozifanya katika kuleta maendeleo kwa mkoa wa Arusha katika nyanja mbalimbali hasa upatikanaji wa maji safi, ujenzi wa barabara,uboreshaji wa huduma za afya na kuboresha elimu kwa ujumla.
Aidha, amesema mkoa wa Arusha umeendelea kuleta maboresho zaidi katika sekta ya elimu kwa kuandaa utaratibu wa kutunga mtihani mmoja kwa shule zote za mkoa wa Arusha,ambapo awali kila shule ilikuwa inaanda mitihani yake.
Rais Magufuli yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 2 ambapo alitokea mkoani Manyara huko  alikabidhiwa ukuta wa machimbo ya Mirerani na sasa anaendelea na ziara  yake mkoani Arusha.


Kikosi cha polisi chakuzuia ghasia(FFU) kikionyesha namna yakuzuia maandamao mbele ya Rais Magufuli (hayupo pichani) katika sherehe za uzinduzi wa kituo cha polisi  cha utalii,Arusha.


0 comments:

Post a Comment