Yamesemwa hayo na Rais wa jamuhuli ya muungano wa
Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alipohudhuria sherehe za kusimikwa kwa
askafu mkuu wa jimbo la Arusha mhashamu Isaac Imani.
Amesema amani ndio kitu pekee kitakachoweza kuleta
mshikamano,upendo na maendeleo katika nchi yetu.
Watanzania wote wanapaswa kufahamu kuwa amani ndio kitu
wanachotakiwa kukitunza na kukiheshimu,hivyo wasikubali baadhi ya watu
wawashawishi kuipoteza amani hiyo.
Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini na
madhehebu yote ya hapa nchini katika kudumisha amani na kuleta maendeleo ya
nchi kwani serikali haina dini na inahudumia watu wake wote.
Aidha, katika kuendeleza ujenzi wa kanisa jipya la jimbo
la Arusha ameaidi kuchangia mifuko 300 ya simenti,pia ametoa zawadi ya Ng’ombe
2 kwa askofu aliyemaliza mda wake
Josephati Luisi Lweburu kama ishara yakumshukuru kwa ushirikiano wake
kwa serikali.
Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
amewataka wananchi wa Arusha waendelee kufuata sheria na taratibu za nchi,hii
itasaidia kuepuka migongano ya hapa na pale inayojitokeza mara kwa mara.
Alimshukuru askofu aliyemaliza mda wake wa utumishi askofu
Josephati Lweburu kwa ushirikiano wake mkubwa aliouwonyesha kwa uongozi wa
mkoa.
Askofu mpya Isaac Amani amesema uongozi ni dhamani
inayoitaji mshikamano baina ya wanaoongozwa na wanaoogonza.
Amesema ushirikiano na kusikilizana ndio itasaidia
kufanya kazi kwa bidii na kwa umoja.
Aidha, amesema kama nchi tusiruhusu ufa wowote katika
nchi yetu bali tukae kwa upendo na amani.
Magufuli alihudhuria sherehe za kusimikwa kwa askofu
mkuu wa jimbo la Arusha mhashamu Isaac Amani baada ya aliyekuwa askofu wa jimbo
hilo Josephati Lweburu kumaliza mda wake wa utumishi.
Rais Magufuli akiwa na mkwe Mama Janeth wakiwasamilia baadhi ya maaskofu na Mapadre walipohudhuria sherehe za kusimikwa kwa askofu mkuu wa jimbo katoriki la Arusha mhashamu askofu Isaac Imani. |
Rais Magufuli akimpongeza askofu mkuu wa jimbo katoriki la Arusha mhashamu Isaac Imani baada yakusimikwa rasmi kuwa askofu wa jimbo la Arusha,katika Kanisa la Mt.Theresia jijini Arusha. |
Mke Rais Magufuli, mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa hongera askofu mteule wa jimbo kuu katoriki la Arusha mhashamu Isaac Imani baada yakusimikwa rasmi katika kanisa la Mt. Theresia jijini Arusha. |
0 comments:
Post a Comment