Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akipanda mti kama ishara ya uzinduzi wa siku ya upandaji miti kimkoa,wilayani Monduli. |
Halmashauri za mkoa wa Arusha zatakiwa kuhakikisha
zinatenga bajeti ya kutosha kusaidia zoezi la upandaji miti.
Yamesemwa hayo na mkuu wa wilaya ya Monduli Theresia
Mahongo alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa
Arusha.
Amesema halmashauri zote zitenge bajeti ya upandaji miti
ya kutosha ili kuongeza lengo la
upandaji miti la mkoa ambalo nikupanda miti
10,500,000 kwa mwaka.
Ambapo kwa mwaka
2014/2015 idadi ya mti milioni 4.9 ndio ilipandwa na iliyopona ni
milioni 4.4 sawa na asilimia 90, mwaka 2015/2016 miti iliyopandwa ilikuwa
milioni 4 na iliyopona ni milioni 3.4 sawa na asilimia 87 na mwaka 2016/2017
miti iliyopandwa ilikuwa milioni 4 na iliyopona milioni 3 sawa na asilimia 76.
Kwa takwimu hizi inaonyesha dhahili kuwa bado juhudi
zinahitajika zaidi katika upandaji miti katika halmashauri zetu ili tuweze
kufikia lengo la miti milioni 10 kwa mwaka.
Amesema faida kuwa inapatikana wanapopanda miti katika
maeneo yao hasa utunzani wa mazingira na kuzuia mmomonyoka wa ardhi na hata upatikanaji
wa mvua unakuwa mzuri.
Amesisitiza zaidi kwa halmashauri ambazo bado
zinalegalega katika kupanda miti kama halmashauri ya Longido kuhakikisha
inaongeza juhudi za upandaji miti kila mwaka.
Afisa misitu wa Mkoa bwana Julius Nobat Achiula amesema
Changamoto kubwa zinazojitokeza katika kufanikisha zoezi hili kila mwaka ni
mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri ukuaji wa miti iliyopandwa.
Pia kuna uharibifu unaotokana na wanyama kupita katika
maeneo yaliyopandwa miti na mwamko mdogo kutoka kwa wananchi katika upandaji wa
miti.
Amesema kutokana na Changamoto hizo tayari mkoa
umeshaanza juhudi za kutoa elimu na kuhamasisha juu ya upandaji miti kupitia
kamati za mazingira za vijiji na kata.
Halamshauri inayoongoza kwa kufanya vizuri kwenye zoezi
hili la upandaji miti kwa mkoa wa Arusha ni halmshauri ya Arusha ambapo kwa
mwaka 2016/2017 walifanikiwa kupanda miti milioni 1.1 na halmashauriya Longido
ndio iliyofanya vibaya katika zoezi hili kwa kupanda miti 25,810 kwa mwaka
2016/2017.
Maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa yamefanyika
katika mkoa wa shinyanga na kwa mkoa wa Arusha yamefanyika katika kijiji cha
Selela wilayani Monduli.
0 comments:
Post a Comment