Ameyasema hayo alipohudhuria ibada ya kumbukumbu ya kifo
cha hayati Edward Moringe Sokoine nyumbani kwake wilayani Monduli.
Amesema hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa mkweli na mwadilifu katika utumishi wake na
kwa jamii yake,hivyo sisi kama viongozi wa awamu hii ya tano hatuna budi
kuendelea kuiga mfano wake.
“Jukumu letu nikuendelea kumuombea hayati Sokoine kwani
matendo yake bado tunayaishi na yataendelea kutuongoza.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombelezo cha kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine nyumbani kwake Monduli. |
Amesisitiza kuwa hayati Sokoine alijikita katika
kuwajibika kwa watumishi wa umma na serikali ya awamu hii nayo imeweza
kurudisha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Pia hayati Edward Sokoine alianzisha falsafa ya ‘Kilimo
ni uti wa Mgongo’ na sasa serikali inaendeleza falsafa hiyo kwa kujikita katika
kilimo cha uzalishaji chenye tija.
Amesisitiza kuwa
hayati Sokoine alikuwa msikivu kwa
kusikiliza kero mbalimbali za watu na hakuwa na kinyongo wala tabia ya kujilimbikizia
mali hivyo ni mfano wakuingwa na watanzania wote.
Waziri Mkuu Kassim Majali akiwaongoza baadhi ya viongozi katika misa ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli. |
Amesema alikuwa mtu wakubuni mbinu mbalimbali za kusaidia
watu wake katika jamii yake na hii imesababisha kuendelea kukumbukwa na wengi
kwa upendo wake huo.
Akitoa neno la shukrani Lembrisi Kivuyo kwa niaba ya
familia ya hayati Edward Moringe Sokoine,amesema serikali imekuwa ikiwa karibu
sana na familia hiyo tangu kuondokewa na mpendwa wao hivyo ameishukuru sana
serikali kwa hilo.
Amesema familia yao itaendelea kuunga mkono serikali ya
awamu ya tano kwa juhudi zake zinazofanya katika kuleta maendeleo kwa nchi.
Hayati Edward Moringe Sokoine alifarikia Aprili 12, 1984
akiwa kama waziri
mkuu wa Tanzania wa tatu akimfuatia hayati Rashidi Mfaume
Kawawa na kila mwaka familia yake hufanya ibada hiyo ya kumbukumbu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa dini mbele ya kaburi la hayati Edward Moringe Sokoine alipoweka shada la mauwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo chake,mkoani Arusha. |
0 comments:
Post a Comment