Waziri wa Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Luhanga Mpina,
ameiagiza bodi ya maziwa kwa kushirikiana na baraza la kilimo Tanzania kuandaa
maonyesho ya kimataifa ya wiki ya maziwa badala kila mwaka kuadhimisha
yakitaifa tu.
Ameyasema hayo alipokuwa akufungua maonyesho ya 21 ya
wiki ya maziwa kitaifa, yaliyofanyika katika viwanja vya Themi Njiro jijini
Arusha.
Amewataka kuendelea kusimamia sheria na kanuna za maziwa
zinazotumika katika kila nchi, kwani soko la maziwa linapanuka kwa kasi sana.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuhakikisha
inabadilisha sheria na kanuni ambazo zinaonekana hazina tija katika sekta hiyo,
hii itasaidia sana katika uboreshaji wa soko la maziwa ndani na nje ya nchi.
Amewahasa wafugaji waendelee kutumia ufugaji wa kisasa
kwani utaongeza uzalishaji wa maziwa kwa wingi nakutoa fursa zaidi za masoko
kwa nchi za nje.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameipongeza sana bodi ya
maziwa kwa kufanikisha madhimisho hayo ya wiki ya maziwa na amewataka
wazalishaji wazingatie zaidi sheria na kanuni za ndani na nje ya nchi ili
kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.
Magreti Kihumbuli mwakilishi kutoka bodi ya maziwa
Kenya, ameishukuru bodi ya maziwa Tanzania kwa kuwapa mwaliko wakushiriki maonyesho
hayo.
Amesema anatagemea kujifunza mambo mengi katika
maonyesho hayo na hata pia waonyeshaji wa Tanzania watajifunza mengi kutoka
kwao na hii itasaidia kuongeza uhusiano bora kati ya nchi hizi.
Luge Kawaga ni mwakilishi kutoka mamlaka ya endelezaji
wa maziwa nchini Uganda, amesema maonyesho hayo yatasaidia kubadilisha elimu
baina ya nchi hizo tatu.
Maonyesho ya wiki ya maziwa kitaifa yanafanyika mkoani Arusha
kwa siku 3 ambapo makapuni takribani 40 yakiwemo ya kigeni yameweza kushiriki maonyesho
hayo.
0 comments:
Post a Comment