|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mbunge wa jimbo la Longido Dkt. Steven Kiruswa, wakishirikiana na wananchi wa kata ya Ketumbeini kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo,wilayani Longido.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema wananchi wa
kata ya Kimokouwa na Namanga kwa ujumla hawana haja yakupata matibabu tena kutoka
nchi jirani ya Kenya.
Aliyasema hayo alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha
Eworendeke katika kata ya Kimokouwa wilayani Longido.
Gambo amesema kwa mda mrefu sana wananchi wa Namanga kwa
ujumla walikuwa wanapata hadha yakufuata huduma ya matibabu Longido mjini au
nchi jirani ya Kenya na hivyo kufanya wagonjwa wengi kutembea umbali mrefu.
Amesema kituo hicho cha afya kimepata mgao wa shilingi
milioni 700 kutoka serikalini na wananchi wanachangia nguvu kazi katika
kukijenga na mpaka sasa kiasi cha milioni 400 ndio kimeshatumika na ujenzi unaendelea.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenabor kitakacho gharimu kiasi cha milioni 200 mpaka kukamilika.
Gambo amesema mbali na serikali kutoa kiasi hicho cha
fedha bado bajeti ya ununuzi wa madawa umeongezwa kutoka bilioni 31 hadi
bilioni 269 kwa mwaka huu wa fedha, na hii itasaidia huduma ya madawa
kupatikana kiurahisi katika kila kituo cha afya na hospitali zote nchini.
Kituo cha afya cha Eworendeke kinatarajia kukamilika
Agosti 2018 na huduma zote zitapatikana zikiwemo huduma za upasuaji na x-ray, hivyo itarahisisha
matibabu kwa wananchi wote wa Namanga.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo,amesema asilimia
27 ya wajawazito walikuwa wanajifungulia katika vituo vya afya kwa wilaya nzima
na idadi imeongezeka kufikia asilimia 35.
Chongolo amesema ongezeko hili litasaidia kupunguza vifo
vya mama na mtoto katika wilaya yake.
|
|
Ujenzi wa kituo cha afya cha Eworendeke Namanga unaondelea na kituo kitagharimu kiasi cha milioni 700 fedha kutoka serikalini,kituo kipo wilayani Longido.
Mgaga mkuu wa Mkoa Dokta Vivian Wonanji,amesema serikali
imeshatenga kiasi cha fedha cha milioni 200 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa kwa
vituo vyote vya afya na hospitali kwa mkoa mzima na anaendelea na zoezi la kuongeza
watumishi katika sekta ya afya.
Amesema agizo la serikali ni kuhakikisha vituo vyote vya
afya vinakuwa na huduma ya x-ray, hivyo katika kituo hicho wanajenga chumba
maalumu kitakachotoa huduma hiyo kwa wananchi wote wa Namanga.
Akitoa shukurani zake za dhati kwa serikali bwana Hassan
Hamis ambae ni mkazi wa Namanga amesema kweli kituo hicho cha afya kitasadia
kuondokana na hadha waliyokuwa wanaipata kufuata matibabu kwa umbali mrefu, na
pia itapunguza vifo vilivyokuwa vinatokana na umbali huo.
Gambo anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Longido
ambapo ametembelea kituo kingine cha afya cha
Engarenaibor kilichogharimu kiasi cha milioni 200, pia ameshiriki ujenzi
wa kituo cha afya cha kata ya Ketumbeine.
|
0 comments:
Post a Comment