Friday, May 5, 2017

RC GAMBO AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WA MKOA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.     


Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.

Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.

Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji  wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.

Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.

Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.

Nae katibu tawala wa mkoa  Richard  Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.

Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.

Mkuu  wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha.

0 comments:

Post a Comment