Katibu mkuu wa wizara ya habari,Utamaduni,sanaa na
michezo, Suzan Mlawi amesema,Taifa lisilo na utamaduni ni taifa linalokufa na
kutoa kizazi kisichoweza kuenzi na kuthamini mila na desturi zao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua tamasha la Urithi wa
Utamaduni katika mkoa wa Arusha lililoanza Octoba 8, 2018 hadi Octoba 13 katika
viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
“Nimefarijika kuona tamasha hili litakuwa linafanyika
kila mwaka, kwani litatoa nafasi kubwa sana kwa watanzania kujifunza tamaduni
mbalimbali na pia litaenzi mila na desturi zetu kwa kiasi kikubwa”,alisema.
Amesema kupitia tamasha hili anategemea kuona ukuaji wa
uchumi kwani bidhaa nyingi za asili zitapata masoko,kufufua mila na desturi
zilizokufa kwa vijana wa sasa.
Mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi Pro.Audax Mabula, amesema tamasha hili
lilizinduliwa mnamo Septemba 15,2018 na makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu
Hasan mjini Dodoma na kuendelea Zanzibar,
Dar es Salaam na sasa lipo mkoani Arusha.
Amesema lengo kubwa la tamasha hili ni kuenzi mila na
malikale za Kitanzania kwani ni kwa mda mrefu sasa utamaduni wa watalii ndio umekuwa ukipewa
kipaombele zaidi kuliko huu utalii wa utamaduni.
Tamasha hili la urithi wa utamaduni lilizinduliwa kwa
mala ya kwanza nchini jijini Dodoma na litakuwa likifanyika kila mwaka kwa
mwezi mzima wa Septemba katika mikoa mbalimbali na kwa Mkoa wa Arusha
linafanyika pia katika wilaya ya Karatu.
0 comments:
Post a Comment