Friday, October 5, 2018

UGONJWA WA VIKOPE TISHIO

Viongozi wa Wilaya wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji dawa za ugonjwa wa vikope (Trakoma) kwenye maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha ugonjwa huu unatokomezwa kabisa.

Akitoa rai hiyo alipokuwa akifungua semina ya mpango wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaombele  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, katibu tawala wa mkoa Richard Kwitega amesema ni vizuri viongozi wakajikita kwa nguvu zote katika zoezi hili lakutokomeza ugonjwa wa vikope kwenye maeneo yao.

“Ni rai yangu kwenu viongozi wote wa Wilaya na halmashauri kuhakikisha mnasimamia vyema zoezi hili lakutokomeza ugonjwa huu wa vikope katika maeneo yenu”.
Lengo la serikali nikutumia rasilimali chache kuthibiti magonjwa haya ambayo yanaonekana hayapewi kipaombele katika jamii yetu hivyo kila halmshauri ihakikishe inatenga fedha zakutosha zakusaidia upasuaji wa vikope.
Wilaya ya Karatu na halmashauri ya Arusha zimejitaidi kuhakikisha zimetokomeza ugonjwa wa vikope lakini bado katika halmashauri ya wilaya ya Longido na Ngorongoro, nguvu zaidi zinaitajika katika maeneo haya.

Kwa mkoa wa Arusha watu takribani 1076 wameshafanyiwa upasuaji wa vikope katika halmshauri zote za wilaya na magonjwa yanayoongoza katika mkoa huu ni ugonjwa wa Kichocho ,Minyoo ya Tumbo na vikope.

Amewataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoipata katika mafunzo hayo wakaitumie vizuri katika kutokomeza magonjwa hayo kwenye maeneo yao.
Nae mratibu wa magonjwa yalisiyopewa kipaombele  kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto Dokta Upendo Mwingira, amesema takribani magonjwa 17 yasiyopewa kipaombele yapo katika bara la Asia, Amerika ya Kusini na Kusini mwa jangwa la Sahara.

Amesema magonjwa mengine ambayo hayapewi kipaombele ni AIDS, TB, Malaria, Kuumwa na nyoka,Matende, Mabusha, Usubi na Ukoma.
Amezitaja athari mbalimbali zinazotokana na magonjwa haya ni kama mgonjwa kupata ulemavu wa mda mrefu, Udumavu kwa watoto,kupunguza uwezo wa kufanya kazi,unyanyapaaji, kansa ya kibofu cha mkojo, upofu na presha ya ini.


Akitoa taarifa fupi ya ugonjwa wa vikope kwa mkoa wa Arusha Dokta Mwanahawa Kombo kutoka hospitali ya Mkoa Mt. Meru, amesema jumla ya wagonjwa 1076 wameshapasuliwa vikope na halmashauri ya Monduli imefanya vizuri katika kukabiliana na ugonjwa huu kati ya halmashauri 2 za Longido na Ngorongoro.
Semina hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa elimu na takwimu sahihi za hali  halisi ya magonjwa yasiyopewa kipaombele nchini.

Semina hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa elimu na takwimu sahihi za hali  halisi ya magonjwa yasiyopewa kipaombele nchini

0 comments:

Post a Comment