Yamesemwa hayo na katibu tawala wa Mkoa Richard Kwitega
kwa niaba ya mkuu wa mkoa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya namna ya
upangaji wa bajeti ya lishe katika mkakati wa lishe Kitaifa, amesema hali ya
udumavu katika mkoa si nzuri sana upo kwa asilimia 36.
Amesema wahanga wakubwa ni watoto na wanawake ambapo
watoto wengi wanaudumavu wa akili na mwili na wanawake wajawazito hujifungua
watoto njiti au hupoteza maisha kabisa.
Hali za watoto kwa mkoa wa Arusha kwa mwaka 2015/2016 watoto wenye uzito mdogo kwa urefu ni asilimia 6.5 na wenye uzito mdogo kwa umri ni
asilimia 20.1 na watoto 57 kati ya 100 wana upungufu wa damu.
Amesema hali hii pia kwa akinamama wajawazito sio nzuri
kwani wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 17, 14 kati ya 100 wana
upungufu wa damu kwa takwimu za mwaka 2015/2016.
Akisisitiza zaida mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel
Daqarro amesema ifike wakati sasa elimu itolewe kwa kina juu ya ulaji mzuri wa
vyakula mbadala vitakavyo ongeza virutubisho mbalimbali katika mwili badala ya
kutumia madawa kwa wingi.
Amesema vyakula kama mbogamboga, matunda na vyakula vya
nafaka vinavyoongeza madini, vitamin na virutubisho vingine mbalimbali
yanayoitajika mwilini.
Pia, mpango mkakati wa lishe unaitaji bajeti ambayo
utasimamia utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa, amesema mafunzo hayo waliyopatiwa
yatawasaidia kuwa na uwelewa mpana wa namna ya kusimamia shughuli nzima za
lishe katika wilaya zao kwa ufasa.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kutengeneza bajeti
za lishe katika mkoa wa Arusha yaliyosimamiwa
na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yalifanyika
kwa kuhusisha wilaya mbili ya Jiji la Arusha na Arusha Vijiji na kuendelea
katika wilaya nyingine za Meru, Longido,Monduli,Karatu na Ngorongoro.
0 comments:
Post a Comment