Amesema ukosekanaji wa ujuzi ndio changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi kwa sasa, kwani tafiti za mwaka 2014 zinaonesha kuwa 3.5% ya watu wana ujuzi wa juu, 16.6% wana ujuzi wa kati na 76.9 wana ujuzi wa chini kabisa.
Amesema viwango vya kimataifa vinatambua ujuzi katika
12% uwe wa juu,34% wa kati na 54% niwa chini, hivyo nchini yetu bado inakazi
kubwa sana katika kuhakikisha tunafikia kiwango hicho cha kimataifa.
Amewasisitizia vijana wote nchini kuakikisha wanatunza
afya zao kwani bado kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)
kipo kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewataka vijana
wasikubali kutumika na watu kwa mambo mbalimbali kama yakisiasa, amesema vijana
wanatakiwa kuwa makini katika maamuzi wanayoyataka kuyafanya ili waweze kuamua
vitu vyenye tija.
Vijana wakiingia katika viwanja vya chuo cha Patandi kwa Maandamano katika kilele cha siku ya vijana duniani,Arusha. |
Nae Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambae ndie
alikuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ya kilele cha siku ya vijana, amesema
wilaya yake imeshatenga ekari 3000 kwenye eneo la Malula kwa ajili ya uwekezaji
na vijana ndio watapewa kipaombele cha kupewa maeneo hayo.
Ameishukuru serikali ya Mkoa kwa kuleta maonesha hayo
katika wilaya yake na amesema wananchi wa Arumeru wamefurai na wamepata elimu
ya kutosha.
Maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa yalianzishwa
rasmi na umoja wa mataifa kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana kujadili maswala
mbalimbali yanayowahusu na kuyatafutia majibu na huanzimishwa kila mwaka Agosti
12 ambapo mwaka huu 2018 yameadhimishwa Mkoani Arusha.
Mheshimiwa Antony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya DSW bwana Peter Owaga katika kilele cha siku ya vijana,Arusha. |
0 comments:
Post a Comment