Baadhi ya mafundi wakiwa kazini kwenye ujenzi wa kituo cha afya Nduruma,wilayani Arusha. |
Katika kutekeleza
maelekezo ya uboreshaji na ukarabati wa vituo vya afya nchini, Mkoa wa
Arusha amefanikiwa kuboresha vitua vya afya viwili kwa awamu ya kwanza.
Akitoa taarifa fupi
ya maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo,Mganga mkuu wa Mkoa Dr.Vivian Timothy
Wonanji, amesema mpaka sasa kwa mkoa wa Arusha zoezi hili linaendelea vizuri na
kwakasi kubwa.
Awamu ya kwanza,
Mkoa ulipata kiasi cha bilioni 1.4 kwa ujenzi wa vituo viwili vya afya,ambapo ni
kituo cha afya cha Nduruma kilipata kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili ya
ujenzi na milioni 200 kwaajili ya ununuzi wa vifaa na kituo cha afya cha Kambi
ya Simba kimepata milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 za ununuzi wa
vifaa.
Amesema kituo cha
fya cha Nduruma kilichopo katika halmashauri ya Arusha kinaendelea na ujenzi wa
majengo matano na mpaka sasa yapo katika hatua ya ukamilishaji,majengo hayo
yakiwemo wodi ya wazazi na jengo la upasuaji.
Kituo cha pili ni
Kambi ya Simba kilichopo katika Wilaya ya Monduli, ambapo mpaka sasa ujenzi
unaendelea wa majengo nane yakiwa kwenye hatua ya upauwaji.
Aidha,amesema katika
awamu ya pili ya ujenzi wa vituo vya afya, mkoa wa Arusha umeshaanza maandalizi
yake kwa uundaji wa kamati mbalimbali zakusimamia shughuli nzima na kiasi cha
shilingi bilioni 1.2 zimeshatolewa na benki ya dunia kwa ujenzi wa vituo vya
afya 3 .
Wilaya ambazo
zimepata fedha hizo ni, Wilaya ya Ngorongoro katika ujenzi wa kituo cha afya
cha Sakala, Wilaya ya Monduli kituo cha afya cha Mto wa Mbu na Wilaya ya
Longido ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenaiobor,ambapo kila kituo kitapatiwa
kiasi cha shilingi milioni 400.
Pia, serikali imetoa
fedha za ukarabati wa vituo vya afya mkoani Arusha, kikiwemo kituo cha afya cha
Murieti,kimepata kiasi cha milioni 700.
Kituo vingine ni
kituo cha afya cha Usa liver ambacho kimepata kiasi cha shilingi milioni 700
kwaajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji kwa wakinamama.
Kituo cha afya cha
Ololiendeki wilayani Longido nacho kimepata kiasi cha milioni 700 kutoka
serikalini.
Dokta Wonanji
amesema, mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya kwa mkoa wa Arusha, awamu ya
kwanza vituo vya afya 2 vimeweza
kunufaika, na awamu ya pili utakamilishwa kwa ukarabati wa vituo vya afya 6 na
kupelekea mpango huu kukarabati vituo vya afya 8 kwa mkoa mzima wa Arusha.
Mpango huu wa
ukarabati wa vituo vya afya upo katika awamu mbili,yakwanza ilianza rasmi
Septemba,2017 na utakamilika Januari,2018,ambapo awamu ya pili umeanza Januari
2,2018 na utakamilika Aprili,2018.