Mkuu wa wilayaya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro akizungumza na baadhi ya vijana wa jiji la Arusha wakati akifungua mdahalo wa vijana kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro
amefungua mdahalo wa vijana wa jijini Arusha kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo, uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha(ATC),mdahalo ulikuwa na
lengo lakutoa elimu kwa vijana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo
katika Mkoa wa Arusha.
Daqarro aliwahamasisha vijana kujiunga na vikundi
mbalimbali vilivyosajiriwa ili waweze kupata mikopo ya serikali itakayowasaida
katika shughuli mbalimbali zakuinua uchumi wao badala ya wao kukaa vijiweni
nakulalamika hakuna ajira.
“Ni vema vijana mkajiunga kwenye vikundi vya watu 8 hadi
30 na mkavisajiri ili muweze kupata mikopo kutoka serikalini kuliko kukaa
vijiweni nakusubiri ajila ziwafuate au kulalamika hakuna ajira”.
lisisitiza kuwa vijana pia watafute fursa kwenye soko
la jumuiya ya afrika masharika kwani wakilala wao ndio watageuzwa kuwa soko
kwasababu fursa zote zitachukuliwa na wageni.
Pia amewahasa wasipendi urahisi wamaisha kwakutaka
mafanikio haraka kwa njia zisizo halali kwani ndio zinawapelekea wajiingize
katika biashara harama kama zakuuza na kutumia madawa ya kulevya.
Hata hivyo taasisi mbalimbali nazo ziliweza kuonyesha
fursa zilizopo katika taasisi zao ambazo zinawafaa vijana kuwajenga kiuchumi,baadhi
yao walikuwa ni Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO),Shirikisho la maenyesho ya kilimo(TASO),HAKIKA BANK, Taasisi yamikopo ya mashine (EFTA),VETA na mashirika yanashughulika na
vijana kama DSW, VISION FOR YOUTH (V4Y) na Shirika la kilimo cha mbogamboga,matunda na maua(TAHA).
Akielezea zaidi afisa maendeleo ya vijana,Japhet Kurwa alisema
serikali bado inaendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sera ya vijana
kupitia midahalo kama hivyo ili vijana waweze kufahamu fursa zilizopo serikalini
na waweze kuzichangamkia.
Hata hivyo aliwataka vijana wao wenyewe wajitaidi
kutafuta taarifa sahihi katika ofisi mbalimbali za serikali na hasa ofisi yake
iko wazi kwaajili yao hivyo wasijisikie kama wamesahaulika katika jamii bali
wao hawatakiwi kulala ila nikukamata kila fursa wanayoiyona mbele yao.
Afisa Maendeleo yaVijana wa Mkoa wa Arusha,Japhet Kurwa akiwakaribisha wajumbe wa mdahalo wa vijana katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC). |
Baadhi ya watoa mada wakiwa pamoja na mgeni rasmi wa mdahalo wa vijana,Jijini Arusha. |
Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na shughuli za vijana na vijana mbalimbali waliohudhulia mdahalo wa vijana. |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mdahalo wa vijana uliofanyika Jijini Arusha. |