Ambapo wataalamu wote kutoka mikao mitatu waliweza kuwasilisha hali halisi ya vifo vya mama na mtoto kwa mikoa yao mitatu.
Aidha baada ya taarifa hizo mjadala ulifuata wakuweka malengo na mikakati zaidi itakayoenda kutekelezwa katika mikoa yote mitatu.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na mikoa yote mitatu ni ;kuongeza idada ya maafisa maendeleo ya jamii katika ngazi za kata,kuboresha zaidi mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya.
Pia viongozi wa hospitali wapewe elimu ya uongozi bora iliwaweze kuwaongoza vizuri waliochini yao,kuongeza vifaa tiba na upatikanaji wa damu salama,watumishi waliopo wafanye kazi kwa bidii na kuongeza wateja wa bima ya afya(CHF/TIKA) kwa kila kata.
Akisisitiza zaidi Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara bwana Eliakimu Maswi amewataka watumishi wote wa afya wabadili mitazamo yao juu yakutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuwepo na motisha kwa watumishi wa chini ili kuwapa moyo wakufanya kazi.
Taasisi hii imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali katika tafiti zake wanazofanya kwa upande wa afya nakushirikisha mawazo yao katika vikao vyao wanavyofanya kwa kila kanda kwa lengo lakuboresha hali ya huduma ya fya katika jamii.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha afya chakujadili jinsi yakupunguza vifo vya mama na mtoto, Jijini Arusha. |
Makatibu Tawala wa mikoa mitatu ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara walishiriki pia kikao cha afya chakupinga vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kaskanzini. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Eliakimu Maswi akifunga kikao cha afya kilichojadili jinsi yakuzuia vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kanskazini. |
0 comments:
Post a Comment