Katibu Tawala Msaidizi upande wa elimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya usimamizi wa sheria ya elimu kwa shule binafsi. |
Shule zote binafsi za mkoa wa Arusha zimetakiwa kufuata
sheria ya elimu ya mwaka 2012 ya usimamizi wa upandaji wa
madarasa kwa wanafunzi wa shule hasa za Sekondari.
Akitoa rai hiyo katibu tawala masaidizi upande wa elimu
bwana Gift Kyando, amesema serikali
imeweka utaratibu wa upimaji wa wanafunzi kwa darasa la nne, darasa la
saba,kidato cha pili na kidato cha nne.
“Hakuna utaratibu wakumpima mwanafunzi wa kidato cha
tatu kwenda kidato cha nne kama inavyofanywa na baadhi ya shule binafsi kwa
kuweka wastani wa alama za masomo kwa wanafunzi na ambae hata fikisha kiwango
hicho hufukuzwa shule au kuamliwa kurudia kidato”.
Amesema serikali haitafumbia macho kwa shule yoyote
itakayokiuka sheria hiyo ya elimu nakuwataka wakuu wote wa shule wanaoendesha
shule zao kwa kukiuka utaratibu huo kuacha mara moja na pia amewasihi wazazi
wote waendelee na maandalizi ya watoto wao wanaoingia kidato cha nne bila hofu
yoyote.
Pia amesema serikali itaendelea kuzifuatilia shule zote
za binafsi hasa zilizobainika kukiuka sheria hiyo ili kuhakikisha wanafunzi
hawafukuzwi au kurudia madarasa bila utaratibu uliowekwa na serikali.
Amewataka wazazi wote ambao watoto wao watakataliwa
kuendelea na masomo kwa kigezo cha kikosa wastani wa alama za shule husika,
watoe taarifa haraka katika ofisi za elimu za mkoa wa Arusha
kwa hatua zaidi.
0 comments:
Post a Comment