RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Friday, September 28, 2018

VIONGOZI WA MILA WATAKIWA KIRITHISHA MILA NA DESTURI ZAO.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta. Harrison Mwakyembe akiongozana na viongozi mbalimbali wa mila wa kimaasai na wacheza ngoma, alipohudhuria mkutana wa baraza la viongozi wa koo na rika,jijini Arusha.


Dokta. Mwakyembe akipokea baraka kutoka kwa viongozi wa kimila la kimaasai katika mkutano wao na kiongozi huyo.


Waziri  Dokta. Mwakyembe akivalishwa zawadi ya mgololi kama ishara yakusimikwa kuwa mmoja wa wazee wa kabila hilo la Kimaasai,Arusha.


Waziri Mwakyembe akipokea fimbo kutoka kwa kiongozi wa mila kama ishara ya kuwa mmoja wao kwenye kabila la Maasai,Arusha.




Tuesday, September 25, 2018

TATIZO LA KUPOTEZA KUMBUKUMBU NI UGONJWA NA SIO KAWAIDA KWA WAZEE




Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza umeweza kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 60 zoezi hili limefanyika katika hospitali ya mkoa Mt.Meru.

Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo yaliambatana na upimaji wa magonjwa mengine kama Kisukari, Presha na Uzito, mwanasaikolojia kutoka hospitali ya Mkoa Mt.Meru bwana Ssenku Shafic Mohamed, amesema zoezi hilo limechukua mda wa wiki nzima.

Na lengo kubwa lilikuwa nikuwapima wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ili wajitambue hali yao ya kumbukumbu na magonjwa mengine yasiyoambukiza kama Kisukari,Presha na Uzito.

Aidha, kutokana na zoezi hilo bwana Ssenku amesema wameweza pia kugundua magonjwa mengine kama mtoto wa jicho na tezi dume kwa wazee wanaume.

“Katika hali ambayo hatukitarajia tumeweza kugundua pia ugonjwa wa mtoto wa jicho ambapo kati ya wagonjwa 10 waliokuja hapa watatu kati yao walikuwa wamegundulika na tatizo hilo na pia  ugonjwa wa tenzi dume ambapo kati ya wagonjwa 10 wawili wamegundulika na tatizo hilo”.


Amesema wamefanikiwa pia kutoa ushauri wa vyakula sahihi vinavyowafaa wazee na aina ya mazoezi ili kuhakikisha afya zao zinaimarika na wanajikinga na magonjwa mbalimbali hasa la kupoteza kumbukumbu ambalo lina sadikika ni kawaida kwa wazee lakini kitaalamu ni ugonjwa ambao ukipatiwa matibabu mapema hospitali unatibika.

Maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Septembea 21 duniani na kwa mwaka huu Tanzania kupita mkoa wa Arusha imeadhimisha siku hii kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na nchi nyingine kama vile Mauritius, Nigeria, Zimbabwe, Madasca na Tunisia.

Friday, September 14, 2018

MILIONI 469 ZATUMIKA KATIKA UJENZI WA KITUO CHA FYA

Jengo la kituo cha afya kata ya Mto wa Mbu wilayani Monduli,kilichojengwa na serikali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi.



Milioni 469 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya Mto wa Mbu wilayani Monduli.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mganga mkuu wa kituo cha afya Dr. Emma Agostino Msofe, amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2017 baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400.

Pia fedha nyingine zimetoka halmashuri kiasi cha shilingi milioni 30 na wananchi  wamechangia milioni 39.

Ujenzi wa kituo hicho cha afya unaendelea na mpaka sasa majengo yaliyojengwa ni  jengo la upasuaji, jengo la wazazi,jingo kufulia,nyumba ya utumishi,vyoo vya nje na matenki ya kuhifadhia maji.

Amesema kituo hicho cha afya kitawasaidia wananchi kupata huduma bora za afya na katika mazingira bora.

Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu. Charles Francis Kabeho, amesema wananchi wanatakiwa kukitunza kutuo hicho kwa umakini na pia amewataka watumishi watoe huduma bora na kwa weridi kwa wananchi.


Mwengi wa Uhuru ulianza mbio zake mkoani Arusha Mnamo Septamba 12 katika wilaya ya Ngorongoro kisha wilaya ya Karatu na sasa unaendelea katika wilaya ya Monduli.

Kiongozi wa mbio za Kitaifa ndg. Charles Francis Kabeho, akizundua kituo cha afya cha Mto wa Mbu wilayani Monduli.


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Charles Kabeho ( mwenye sare ya gwanda) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Monduli wakitoka kizindua mradi wa kituo cha afya cha mto wa Mbu.


Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Kabeho akikagua mradi wa kuchakata chakula cha mifugo klatika kijiji cha Mungere kata ya  Esilalei wilayani Monduli.


Thursday, September 13, 2018

MWENGE WILAYANI KARATU

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Mfaume Taka akimkabidhi Mwenge wa uhuru mkuu wa wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya mwenge wilayani humo.

Wakwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo akishuhudia uzinduzi wa nyumba za walimu 6/1 katika shule ya sekondari Baray ujenzi wa nyumba hizo zinakadiriwa kuwa zaidi ya milion 141 kwa ushirikiano na wananchi.

Nyumba mpya ya waalimu 6 by one shule ya sekondari Baray iliyopo wilayani karatu iliyo zinduliwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ndg: Charles F. Kabeho wilayani humo.


Katikati ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Taifa 2018 Ndg:Charles Kabeho akizundua mradi wa shamba la kilimo cha vitunguu katika kijiji Cha Dofa wilayani karatu.



Baada ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg:Charles Francis Kabeho kukamilisha ziara ya mwenge wilaya ya ngorongoro ambapo katika wilaya hiyo miradi 6 imezinduliwa na kiongozi huyo.

Miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa vyoo chenye matundu 10,bweni la wanafunzi wa sekondari,maabara ya kisasa ya kemia na fizikia katika shule ya nainokanoka,barabara ya kiwango cha changarawe kutoka Eneo la Errikepus mpaka nainokanoka,mradi wa maji safi na salama pamoja josho la kisasa kwa ajili ya mifugo katiaka hiyo na vijiji jirani.

Septemba 13 kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndg Charles Kabeho anatarajiwa kuzindua na kukagua maendeleo ya miradi zaidi ya 6 kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo.

Katika wilaya ya karatu kijiji cha Dofa amezindua mradi wa Kilimo cha vitunguu katika shamba la bonde la Eyasi na kutembelea shamba la muekezaji mzalendo ndg Gilole katika kijiji cha Qang'ded baray.

Shamba hilo lenye zaidi ya hekari zaidi ya 70 limekuwa chachu ya kujiingizia kipato kwa wananchi ambapo kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo zaidi ya wananchi 200 wamekuwa wakifanya kazi ndogondogo na kujipatia fedha kwa ajili ya kujikimu katika maisha yao ya kila siku.

Miradi mingine inayo tarajiwa kuzinduliwa na kukaguliwa  ni pamoja na uzinduzi wa nyumba za walimu 6 kwa moja shule ya sekondari Baray,kuzindua kikundi cha vijana katika kampeni ya Tuwalinde vijana wetu,kufungua ofisi ya kijiji kwa ajili ya utoaji huduma.

Thursday, September 6, 2018

MWENGE WA UHURU


Mwenge wa uhuru utawasiri katika mkoa wa Arusha Septemba 12,2018 ukitokea mkoani Mara.
Utapokelewa Olduvai Gorge kata ya Ngoile wilayani Ngorongoro.
Ukiwa katika mkoani wa Arusha utakimbizwa katika halmashauri zote 7 za mkoa.
Mwenge utaanzia kukimbizwa katika wilaya ya Ngorongoro,Karatu,Monduli, Longido,Arumeru na kumalizia Jiji la Arusha.
Mwenge ukiwa katika mkoa wa Arusha utakimbizwa umbali wa kilometa 1,114.9.
Utakagua,kuzindua,kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi ipatayo 46 yenye thamani ya kiasi cha shilingi za tz 36,140,912,094.35 (Bilioni thelathini na sita Milioni mia moja Arobaini laki tisa na kumi na mbili na tisini na nne na senti thelathini na tano).
Mwenge utaweka jiwe la msingi miradi 9,4 itafunguliwa,22 itazinduliwa na 11 itakaguliwa katika halmashuri zote.
Mwenge utamalizia kukimbizwa katika wilaya ya Arusha na kukabidhiwa mkoani Manyara Septemba 18,2018 katika wilaya ya Babati.