Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza umeweza kuadhimisha
siku ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 60
zoezi hili limefanyika katika hospitali ya mkoa Mt.Meru.
Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo yaliambatana na
upimaji wa magonjwa mengine kama Kisukari, Presha na Uzito, mwanasaikolojia
kutoka hospitali ya Mkoa Mt.Meru bwana Ssenku Shafic Mohamed, amesema zoezi
hilo limechukua mda wa wiki nzima.
Na lengo kubwa lilikuwa nikuwapima wazee wenye umri
kuanzia miaka 60 na kuendelea ili wajitambue hali yao ya kumbukumbu na magonjwa
mengine yasiyoambukiza kama Kisukari,Presha na Uzito.
Aidha, kutokana na zoezi hilo bwana Ssenku amesema
wameweza pia kugundua magonjwa mengine kama mtoto wa jicho na tezi dume kwa
wazee wanaume.
“Katika hali ambayo hatukitarajia tumeweza kugundua pia
ugonjwa wa mtoto wa jicho ambapo kati ya wagonjwa 10 waliokuja hapa watatu kati
yao walikuwa wamegundulika na tatizo hilo na pia ugonjwa wa tenzi dume ambapo kati ya wagonjwa
10 wawili wamegundulika na tatizo hilo”.
Amesema wamefanikiwa pia kutoa ushauri wa vyakula sahihi
vinavyowafaa wazee na aina ya mazoezi ili kuhakikisha afya zao zinaimarika na
wanajikinga na magonjwa mbalimbali hasa la kupoteza kumbukumbu ambalo lina
sadikika ni kawaida kwa wazee lakini kitaalamu ni ugonjwa ambao ukipatiwa
matibabu mapema hospitali unatibika.
Maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Septembea 21
duniani na kwa mwaka huu Tanzania kupita mkoa wa Arusha imeadhimisha siku hii
kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na nchi nyingine kama vile Mauritius,
Nigeria, Zimbabwe, Madasca na Tunisia.
0 comments:
Post a Comment