RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Tuesday, December 4, 2018

LIPENI KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA-MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa kina wa sababu inayosababisha wafanyabiashara kutokulipa kodi.

Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru.

Magufuli amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanawatumia wafanyabiashara wadogo (wamachinga) kuwauzia bidhaa zao ingali wao wanafunga maduka yao kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.

Nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi hata mradi huu wa maji niwa mkopo wa riba ya bei nafuu kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na wananchi ndio mtalipa deni hili kwa kulipa kodi.

Amewahasa wananchi kulipa kodi kwa ustawi wa maendeleo ya nchi kwani miradi mingi ya maendeleo inategemea kodi za wananchi,hivyo niwatake wamachinga kutokukubali kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ili wakwepe kodi.

Pia,ameiagiza TRA kuangalia tena viwango vyake vya tozo za kodi kwani huwenda viwango ni vikubwa sana vinavyowafanya wafanyabiashara wengi kukwepa kulipa kodi kwani ni bora kuwa na viwango vidogo ili wengi walipe kuliko viwango vikubwa vinavyowashinda kulipa.

Amesema elimu pia inaitajika kwa wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Magufuli aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji utakaogharimu kiasi cha bilioni 520 mpaka kukamilika na utakuwana na uwezo wakuzalisha lita million 208 kwa siku.



Amewahasa wananchi kulipa kodi kwa ustawi wa maendeleo ya nchi kwani miradi mingi ya maendeleo inategemea kodi za wananchi,hivyo niwatake wamachinga kutokukubali kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ili wakwepe kodi.

Pia,ameiagiza TRA kuangalia tena viwango vyake vya tozo za kodi kwani huwenda viwango ni vikubwa sana vinavyowafanya wafanyabiashara wengi kukwepa kulipa kodi kwani ni bora kuwa na viwango vidogo ili wengi walipe kuliko viwango vikubwa vinavyowashinda kulipa.

Amesema elimu pia inaitajika kwa wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Magufuli aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji utakaogharimu kiasi cha bilioni 520 mpaka kukamilika na utakuwana na uwezo wakuzalisha lita million 208 kwa siku.

Sunday, December 2, 2018

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa jijini Arusha katika kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru.

Amesema wananchi wote ambao wanaishi katika vyanzo vya maji na ambao mradi utawapitia katika maeneo yao watapatiwa maji kwanza wao kabla yakusambazwa maeneo mengine.

Magufuli amesema mradi huu ambao utawanufaisha wananchi wa jiji la Arusha kwa kiasi kikubwa lakini hata pia wananchi wa kata ya Oldonyosambu wilayani Longido pia nao wapatiwe maji kutoka kwenye mradi huo.


“Jana nimesimamishwa  njiani na wananchi wa Oldonyosambu na kero yao kubwa ilikuwa ni ukosefu wa maji safi kwani wanayoyatumia sasa yama madini ya Floride kwa wingi hivyo yanawaadhiri sana wao na watoto wao.”
 Amesema fedha zilitumika katika ujenzi wa mradi huo wa maji ni mkopo wa riba nafuu kutoka Benk ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), hivyo wananchi wote wanajukumu la kulilipa deni hilo.

Magufuli amewataka wakandarasi wa mradi huo ambao wapo 10 wafanye kazi kwa bidii usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika ifikapo mwanzoni mwa Juni 2020 na wananchi waweze kupata maji kwa haraka.
Waziri wa maji na umwagiliaji Pro Makame Mbalawa amesema, hitaji la maji kwa mkao wa Arusha ni lita milioni 94 kwa siku lakini mradi huo unauwezo wakuzalisha lita milioni 208 kwa siku hivyo  ni zaidi ya mara 4 ya uhitaji wa Mkoa.
Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na taka Arusha Enginia Ruth Koya amesema, mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 520.
Amesema mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 208 kwa siku tofauti na hali ya sasa ambayo ni lita milioni 40 kwa siku huzalishwa sawa na asilimia 42 na hitaji la mkoa ni lita milioni 94 kwa siku.

Koya amesema kutokana na ongezeko hilo la uhitaji wa maji wa takribani asilimia 100 hadi ifikapo 2020 mkoa wa Arusha utakuwa na uwezo wakuwahudumia watu takribani milioni 1.

Mbali na mafanikio hayo amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ugumu wa kupata njia zakulaza mabomba hasa katika maeneo ambayo hayajapimwa,pia gharama kubwa za fidia wanazopaswa kuwalipa wananchi.

Rais Magufuli amefanya ziara yake katika mkoa wa Arusha kwa siku 2 kuanzia Desemba 1 hadi Desemba 2,2018 nakuweza kufungua kituo cha malipo ya forodha cha pamoja Namanga wilayani Longido na kumalizia na uwekaji jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji safi na mazingira wa jijini Arusha.


MAGUFULI NA KENYATA WAFUNGUA KITUO CHA FORODHA CHA PAMOJA


Kituo cha forodha cha mpaka wa Namanga mkoani Arusha kinatarajia kukusanya mapato ya kiasi cha bilioni 53 kwa mwaka 2019.

Yamesemwa hayo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua kituo cha pamoja cha forodha kati ya Tanzania na Kenya katika mpaka wa Namanga Arusha.

“Vituo hivi vya huduma ya pamoja vinasaidia kurahisisha usafiri, kukuza biashara na utalii na urahisi kwa wananchi wetu kuvuka mpakani mara  kwa mara.”

Amesema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinachangamoto ya kuwa na vikwanzo vya kibiashara vinavyopeleka uchumi wa nchi hizi kudolola ukilinganisha na mabara mengine kama ya Amerika.

Kutokana na changamto hiyo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikachukua uwamuzi wa kuanzisha vituo vya forodha vitakavyo saidia kukuza biashara kwa nchi husika.

Nae Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyata amesema, kituo hicho kiwe chachu ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza biashara zao kwani wao ndio msingi wa uchumi katika nchi zetu.
Kenyata amesema ni wajibu wa watumishi wa kituo hicho kuwasaidia na kuwajali wafanyabiashara hao wadogo na wao wafanyabiashara wafuate sheria za nchi husika na biashara zao ziwe halali.

Amesema jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanafanya biashara kwa haki na uhuru bila ubuguzi wowote.

Gavana wa jimbo la Kajado Joseph Oleleku, alisema ili nchi hizi mbili ziweze kunufaika na fursa za biashara amekuwa akifanya mikutano ya mara kwa mara ili kuhakikisha wafanyabaishara wanapata haki zao na wanafanya biashara zao kwa uhuru.

Akitoa neno la ukaribisho mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema,Mkoa umeendelea kuhakikisha usalama wa mpaka huo unaimarika kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza ulinzi wa kutumia mbwa.

Gambo amesema mbali na huduma nzuri iliyopo katika mpaka huo kuna changamoto ya ukosefu wa scanna kwa ajili ya ukaguzi wa magari makubwa, ukosefu wa huduma ya upimaji wa ubora wa bidhaa  zinazoingia na kutoka mpakani.

Magufuli yupo katika ziara ya siku 2 mkoani Arusha ambapo amefungua kituo cha pamoja cha forodha na ataweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji katika jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.