Kituo cha forodha cha mpaka wa Namanga mkoani Arusha kinatarajia kukusanya mapato ya kiasi cha bilioni 53 kwa mwaka 2019.
Yamesemwa hayo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua kituo cha pamoja cha
forodha kati ya Tanzania na Kenya katika mpaka wa Namanga Arusha.
“Vituo hivi vya huduma ya pamoja vinasaidia kurahisisha
usafiri, kukuza biashara na utalii na urahisi kwa wananchi wetu kuvuka mpakani
mara kwa mara.”
Amesema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinachangamoto
ya kuwa na vikwanzo vya kibiashara vinavyopeleka uchumi wa nchi hizi kudolola
ukilinganisha na mabara mengine kama ya Amerika.
Kutokana na changamto hiyo nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki zikachukua uwamuzi wa kuanzisha vituo vya forodha vitakavyo saidia
kukuza biashara kwa nchi husika.
Nae Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyata amesema,
kituo hicho kiwe chachu ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza biashara
zao kwani wao ndio msingi wa uchumi katika nchi zetu.
Kenyata amesema ni wajibu wa watumishi wa kituo hicho
kuwasaidia na kuwajali wafanyabiashara hao wadogo na wao wafanyabiashara
wafuate sheria za nchi husika na biashara zao ziwe halali.
Amesema jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wake
wanafanya biashara kwa haki na uhuru bila ubuguzi wowote.
Gavana wa jimbo la Kajado Joseph Oleleku, alisema ili
nchi hizi mbili ziweze kunufaika na fursa za biashara amekuwa akifanya mikutano
ya mara kwa mara ili kuhakikisha wafanyabaishara wanapata haki zao na wanafanya
biashara zao kwa uhuru.
Akitoa neno la ukaribisho mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo amesema,Mkoa umeendelea kuhakikisha usalama wa mpaka huo unaimarika kwa
kiasi kikubwa kwa kuongeza ulinzi wa kutumia mbwa.
Gambo amesema mbali na huduma nzuri iliyopo katika mpaka
huo kuna changamoto ya ukosefu wa scanna kwa ajili ya ukaguzi wa magari makubwa,
ukosefu wa huduma ya upimaji wa ubora wa bidhaa zinazoingia na kutoka mpakani.
Magufuli yupo katika ziara ya siku 2 mkoani Arusha
ambapo amefungua kituo cha pamoja cha forodha na ataweka jiwe la msingi katika
mradi mkubwa wa maji katika jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.
0 comments:
Post a Comment