RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Tuesday, December 28, 2021

Hafla ya Utiliaji wa Saini kati ya Wakala wa maji mjini na Vijijini RUWASA mkoa wa Arusha

 Jumla ya miradi 10 ya maji kati ya 15 yenye thamani takribani billion 5.8  sawa na asilimia 69.4 ya vijiji mkoa wa Arusha vimepata huduma ya maji ambapo malengo ni kufikiwa kwa asilimia 71.3 kufikia vijiji 103 vilivyolengwa.


Hayo yamebainishwa wakati wa Hafla ya Utiliaji wa Saini kati ya Wakala wa maji mjini na Vijijini RUWASA mkoa wa Arusha na wakandarasi walioshinda zabuni iliyofanyika jijini Arusha.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Arusha Injinia Joseph Makaidi Alisema kuwa Miradi hiyo itatekelezwa kwenye wilaya zote za mkoa huo ikiwemo miradi ya Uviko 19 kwenye vijiji 133 huku vituo 101 vya kuchotea maji vikitarajiwa kujengwa kuhudumia watu 25,250 kupunguza idadi ya vijiji 86 hadi 67.

Alisema kuwa serikali kupitia Ilani ya CCM itatekeleza miradi hiyo na ifikapo mwakani mwezi January mikataba minne yenye gharama ya 1.130 kati ya miradi 29 iliyo katika bajeti ya mwaka 2021/2022 itawekwa Saini mbapo mikataba 4 yenye gharama billion 1.676 kwa miradi inayotekelezwa kupitia mpango wa kupambana na Uviko 19.

Awali akiongea baada ya utiliaji Saini Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa Miradi yote inayotekelezwa kwenye wakala za barabara na maji imefanikiwa kupitia Fosce Akaunti hivyo wanayoimani kubwa kwa miradi hiyo kukamilika ndani ya muda uliopangwa.

Alisema kuwa anatoa agizo kwa watendaji wote kuona wajibu wao kufanikisha miradi itakayoelekezwa kuimaliza kwa muda na kuisimamia ipasavyo ili kuwasogezea huduma wananchi.

“Niwaombe wote tushirikiane kama tulivyoshirikiana katika mwaka unaoisha ili kuleta tija na utulivu amani kwa mkoa wetu”

Kwa Upande wake Mhandisi Nyamizi Ntarambe kutoka Kampuni ya Avanced Co ltd alisema sio wageni ila wanaiomba serikali kuendelea kuwaamini na kuwapa zabuni Zaidi zitakazowasaidia kufikia malengo ya kuwa kampuni kubwa kama yalivyo makapuni ya nje.

Mwisho