Hayo yamebainishwa wakati wa Hafla ya Utiliaji wa Saini kati ya Wakala
wa maji mjini na Vijijini RUWASA mkoa wa Arusha na wakandarasi walioshinda
zabuni iliyofanyika jijini Arusha.
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Arusha Injinia Joseph Makaidi Alisema kuwa
Miradi hiyo itatekelezwa kwenye wilaya zote za mkoa huo ikiwemo miradi ya Uviko
19 kwenye vijiji 133 huku vituo 101 vya kuchotea maji vikitarajiwa kujengwa
kuhudumia watu 25,250 kupunguza idadi ya vijiji 86 hadi 67.
Alisema kuwa serikali kupitia Ilani ya CCM itatekeleza miradi hiyo na
ifikapo mwakani mwezi January mikataba minne yenye gharama ya 1.130 kati ya
miradi 29 iliyo katika bajeti ya mwaka 2021/2022 itawekwa Saini mbapo mikataba
4 yenye gharama billion 1.676 kwa miradi inayotekelezwa kupitia mpango wa
kupambana na Uviko 19.
Awali akiongea baada ya utiliaji Saini Mkuu wa Mkoa wa Arusha John
Mongela alisema kuwa Miradi yote inayotekelezwa kwenye wakala za barabara na
maji imefanikiwa kupitia Fosce Akaunti hivyo wanayoimani kubwa kwa miradi hiyo
kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Alisema kuwa anatoa agizo kwa watendaji wote kuona wajibu wao
kufanikisha miradi itakayoelekezwa kuimaliza kwa muda na kuisimamia ipasavyo
ili kuwasogezea huduma wananchi.
“Niwaombe wote tushirikiane kama tulivyoshirikiana katika mwaka unaoisha
ili kuleta tija na utulivu amani kwa mkoa wetu”
Kwa Upande wake Mhandisi Nyamizi Ntarambe kutoka Kampuni ya Avanced Co
ltd alisema sio wageni ila wanaiomba serikali kuendelea kuwaamini na kuwapa
zabuni Zaidi zitakazowasaidia kufikia malengo ya kuwa kampuni kubwa kama
yalivyo makapuni ya nje.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment