RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Tuesday, August 23, 2016

Mwenge wa Uhuru 2016 wapokelewa Mkoani Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya wakiushangilia Mwenge wa Uhuru 2016 baada ya kuwasili eneo la mapokezi katika kijiji cha Ololosokwan.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akikiri kuupokea Mwenge wa Uhuru 2016 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara,Dr.Charles Mlingwa.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa mkoani Arusha mnamo Agosti21,2016 na utakabidhiwa mkoani Kilimanjaro Agosti 28,2016.

Saturday, August 20, 2016

MKUU WA MKOA MPYA WA ARUSHA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Daudi Felix Ntibenda,akisaini hati ya makabidhiano ya ofisi,pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akikabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Daudi Felix Ntibenda.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akisaini hati ya makabidhiano  ya ofisi aliyoipokea kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Daudi  Ntibenda
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akiaga rasmi kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Arusha (hawapo pichani), pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.



Friday, August 19, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Mwenge wa Uhuru 2016

Mwenge wa Uhuru utapokelewa Mkoani Arusha Agosti 21,2016  katika Wilaya ya Ngorongoro kijiji cha Ololosokwani.

Ukiwa katika Mkoa wa Arusha utazunguka katika Halmashauri zote 7 ikianza na Wilaya ya Ngorongoro na kumalizia Wilaya ya Longido.

Mwenge ukiwa Mkoani Arusha utapitia miradi 57 yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni kumi na mbili, milioni mia tisa mia nane kumi na saba elfu mia mbili thelathini,na senti kumi na tatu (12,900,817,230.13).

Aidha miradi 11 itawekewa jiwe la msingi,miradi 14 itafunguliwa,19 itazinduliwa na 13 itatembelewa na kutoa hundi au cheti.

Kisha Mwenge utakabidhiwa Mkoani Kilimanjaro,katika Wilaya ya Siha kijiji cha Matadi mnamo tarehe Agosti 28,2016.Kauli mbiu ya mwaka huu"Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa washikishwe na kuwezeshwa".