Ukiwa katika Mkoa wa Arusha utazunguka katika Halmashauri zote 7 ikianza na Wilaya ya Ngorongoro na kumalizia Wilaya ya Longido.
Mwenge ukiwa Mkoani Arusha utapitia miradi 57 yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni kumi na mbili, milioni mia tisa mia nane kumi na saba elfu mia mbili thelathini,na senti kumi na tatu (12,900,817,230.13).
Aidha miradi 11 itawekewa jiwe la msingi,miradi 14 itafunguliwa,19 itazinduliwa na 13 itatembelewa na kutoa hundi au cheti.
Kisha Mwenge utakabidhiwa Mkoani Kilimanjaro,katika Wilaya ya Siha kijiji cha Matadi mnamo tarehe Agosti 28,2016.Kauli mbiu ya mwaka huu"Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa washikishwe na kuwezeshwa".
0 comments:
Post a Comment