Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya siku yakudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu. |
Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoo,Ummy
Mwalimu amezindua mashine zakisasa (molekyula) zakupima ugonjwa wa kifua kikuu
ambazo zitatumika katika hospitali zote za rufaa nchini na ikiwa ni siku yakudhibiti
ugonjwa wa kifua kikuu duniani.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Arusha nakusisitiza kuwa mashine hizo zinauwezo wakupima wagonjwa 12 kwa siku na zinauwezo
wakugundua usugu wa dawa aliyonao mgonjwa nakupima virusi vya UKIMWI.
Changamoto kubwa ambayo wizara ilikuwa inapata
nikuwagundua wagonjwa wa kifua kikuu mapema nahii imetokana na wagonjwa wengi
kuwa na usugu wa dawa walizokuwa wakitumia na hivyo kuwafanya wasipone kwa
wakati.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya dunia Tanzania
inawagonjwa takribani 1060 wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na
asilimia 30 kati ya wagonjwa 100 tu ndio wanaofika katika vituo vyakupatiwa
tiba.
Mkoa wa Dar es Salaama ndio unaongoza kuwa na wagonjwa
wengi wa kifua kikuu takribani asilimia 22 ikifuatiwa na mikoa ya Mwanza,Mbeya,Morogoro,Shinyanga,Arusha,Mara,Manyara,Tanga
na Kilimanjaro ambayo yenyewe inachangia asilimia 63 ya wagonjwa wote kwa
wagonjwa waliogundulika mwaka 2015.
Mpaka sasa wizara imenunua mashine 70 ambazo wanatarajia
kuzisambaza katika hospitali zote za rufaa za mikoa ikiwa ni awamu ya kwanza na
pia wanampango wakuongeza mashine hizo hadi kufikia 150 ili waweze kubaini
wagonjwa wengi zaidi na hata wale wenye kifua kikuu sugu.
Amesema kutokana na taarifa ya shirika la afya duniani
ya mwaka 2016 Tanzania kila mwaka inashindwa kuwafikia wagonjwa takribani 2400
wenye kifua kikuu sugu na laki moja wenye kifua kikuu.
Hivyo amezitaka halmashauri kuweka mikakati yakubaini
wagonjwa wote wa kifua kikuu kwa kuhakikisha kuwa pindi mgonjwa anapoletwa
hospitali halmashauri ifikie ile kaya ambayo mgonjwa umetoka ili kuwapima
wakazi wote wa kaya hiyo kama kuna ambae ameambukizwa.
Pia amepiga marufuku kwa shule zote za bweni kupokea
mwanafunzi yoyote bila kuwa na fomu maalumu yakutoka hospitali inayoonyesha
vipimo vya magonjwa mbalimbali ambayo mwanafunzi huyo amepimwa ikiwemo ugonjwa
wa kifua kikuu.
Aidha ameagiza wagonjwa wote waliopo kwenye kundi
hatarishi hasa wenye virusi vya UKIMWI, watoto walio chini ya amri wa miaka 5,wamama
wajawazito,wazee,wafungwa, watumiaji wa madawa ya kulevya,watu wenye kisukari
na saratani ni lazima wachunguzwe ugonjwa wa kifua kikuu mara tu wanapofika
kwenye vituo vya tiba.
Pia kundi linguine litakalopimwa ugonjwa huu ni wagonjwa
wanaofika katika idara za nje,cliniki za watu wenye virusi vya UKIMWI na
wagonjwa wote watakaokuwa wamelazwa kwenye hospitali za serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo nae amemwahidi
Waziri Ummy kuongeza ushirikiano katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa kifua
kikuu kwa kushirikiana na wilaya zote za mkoa kuhakikisha kuwa kila kijiji na mtaa
kwenye mikutano yao mikuu ya hadhara watoe elimu ya kutosha na kuhamasisha
wananchi wakapime afya zao kwenye vituo vya afya.
Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto
kila mwaka imekuwa ikiadhimisha siku ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na
mwaka huu siku hiyo ameadhimisha rasmi mkoani Arusha.