Saturday, March 25, 2017

Kamati iliyokuwa ikishughulikia mgogoro wa pori tengefu Loliondo imemaliza kazi yake.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo katikati mwenye shati jeusi na nyeupe akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa eneo la kijiji cha Ololosokwan kilichopo Wilayani Ngorongoro ambapo hiyo ipo kwaajili ya kuingilia maeneo muhimu yanayofaa kwaajili ya uwekezaji,wanyama na binadamu. 


WANANCHI wa Kata Saba Wilayani Ngorongoro ambao wamekubaliana kwa pamoja kwenye mapendekezo yao juu ya kufikia muafaka wa mgogoro wa eneo la Pori Tengefu la Loliondo lenye kilomita 1,500 za mraba
wamesema kuwa endapo maoni yao yatakubaliwa na Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa watakuwa na nidhamu juu ya matumizi bora ya ardhi.
Wakizungumza jana Wilayani hapo wakati wa kikao cha pamoja juu ya
kukubaliana kama eneo hilo la Pori Tengefu Loliondo liwe chini ya
Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori  za Jamii (WMA) au Pori Tengefu (GCA) kwaajili ya wanyama pekee ,wananchi hao walipendekeza kwa pamoja kuwa eneo hilo ni vyema likawa WMA ili jamii iweze kunufaika na maliasili zilizopo.
Wakizungumza jana mbele ya Kamati ya Utatuzi wa Mgogoro huo wa matumzi ya Ardhi ya Pori Tengefu la Loliondo, ambayo inaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wanachi hao walisema ni bora Pori hilo likawa chini ya WMA ili vijiji vinavyozunguuka kata hizo viweze kunufaika na mapato yanayotokana na utalii.

Lakini wengine wakiongozwa na Yanick Ndoinyo walionyesha hofu ya kuwa
na WMA kwa madai kuwa mapato ya kijiji kimoja hivi sasa yatakwenda
kwavijiji vyote vilivyopo kwenye kata saba zilizohusishwa na mgogoro
huo.


“Yani hapa tunatatua mgogoro lakini tunatengeneza mgogoro mwingine
maana ni lazima vijiji vipimwe na tukubaliane kuwa wamoja na kugawana
fedha hofu yangu ni kuwa je vile vijiji vinavyopata hela hapo awali na
hazijulikani zinakwenda wapi vitakubali”.


Alisema ngoja tuone maana tuliyokubali ni sisi kutoa mapendekezo haya
na endapo yatakubaliwa na Waziri Mkuu, Majaliwa hii itatutafuna
wenyewe kwa wenyewe maana hii ngoma bado nzito lakini tunamshukuru Rc Gambo kwa uamuzi huu ila ni lazima tukubaliane juu ya suala hili.
Lakini hoja za kuwa WMA zilipingwa kitaalam na  wahifadhi kutoka
Hifadhi mbalimbali za Taifa,ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori,
Profesa ,Alexander Songorwa alisema kuwa haiezekani mtoto akawa na
mama wawili huku akimaanisha kuwa sheria za wanyamapori na sheria ya
WMA zinakinzana.


“Ili pori hili liweze kuendelea ni lazima kuhakikisha Ikolojia hii
inahifadhiwa kwaajili ya kulisha Hifadhi ya Serengeti pamoja na eneo
hilo la Pori Tengefu kuwa la mazalia ya wanyama hivyo eneo hilo endapo
litaenda WMA hifadhi hii ya Serengeti itakufa”.
Alisema lakini haya ni mapendekezo tu yanaweza yakakubaliwa au la
hivyo kila mtu amesema analitaka kwaajili gani na mwisho wa siku
Waziri Mkuu,Majaliwa atapokea mapendekezo hayo na kasha kutolewa
maamuzi.


Kamati hiyo iiliyoongozwa na Rc Gambo ilikuwa Wilayani Ngorongoro
tangu Machi 15 hadi Machi 21 mwaka huu huku ikikumbana na manadamano ya mara kwa mara kwa wananchi lakini pia wajumbe hao wa kamati walaifanya kazi usiku kucha kushughulikia mgogoro huo kwa kukusanya maoni ya wafugaji,wahifadhi pamoja na wataalam wa ardhi na hatimaye wannachi walitoka na mapendekezo ya kukubali eneo hilo kuwa WMA.


0 comments:

Post a Comment