Mkuu wa Mkoa wa Arusha mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha. |
Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika
katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa
umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa
mkoa.
Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema
viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya
kazi baina yao na watumishi wachini yao.
Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano
inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha
utendaji wa kazi katika maeneo yao na
kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.
Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji
wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.
Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza
maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni
miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi
serikalini.
Nae katibu tawala wa mkoa Richard
Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao
huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya
viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na
maadili ya viongozi na utumishi wa umma.
Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi
kutoka TAMISEMI.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha. |